BAADHI ya wanaume wa Kata ya Kilolambwani wilayani Lindi wamelalamika kuteswa na wake zao kwa kuwashurutisha kufanya kazi kinyume na imani za dini.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao kwenye utambulisho wa mradi wa usawa na jinsia jana, walisema tangu mashirika na asasi za raia zianze kutoa elimu kuhusu haki za wanawake na watoto tabia za wake zao zimebadilika.
Mmoja wa wanaume hao, Farijala Mchopa, alisema elimu inayotolewa na mashirika hayo inakwenda kinyume na imani ya dini zao na hivi sasa wanawake hao hawatawaliki kinyume na matakwa ya dini yao.
Mchopa alishauri asasi inayoratibu mafunzo hayo, Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto cha Lindi (LIWOPAC) na shirika la kimataifa la misaada la OXFA, kuhamasisha zaidi watu wafunge ndoa za serikali usawa unaohubiriwa uweze kukamilika na kukubalika kwa pande zote.
“Usawa huu ili ukubalike, mashirika haya yahamasishe kuanza mchakato wa kuanzisha vyama na mashirika ya kutetea haki za wanaume na kuchangishana mahali,”alisema Mchopa.
Msimamizi wa mradi huo, Romana Colman, licha ya kueleza lengo la mradi huo, alisema asasi za iraia ikiwamo LIWOPAC hazina nia ya kufarakanisha jamii bali haki na usawa ndiyo msingi wa amani na
wapigwe tu hamna namna
ReplyDelete