Wapiganaji wa Rohingya Watangaza Kusitisha Mapigano, Myanmar

Wapiganaji wa Rohingya Watangaza Kusitisha Mapigano, Myanmar
Wa Rohingya wanaishutumu jeshi la Myanmar kwa kuteketeza vijiji vyao - Lakini utawala nchini Myanmar, unasema wanajeshi wake wanakabiliana na "magaidi"Haki miliki ya pichaEPA

Wa Rohingya wanaishutumu jeshi la Myanmar kwa kuteketeza vijiji vyao - Lakini utawala nchini Myanmar, unasema wanajeshi wake wanakabiliana na "magaidi"
Katika taarifa nyingine Asubuhi hii ya leo, waasi wa kiislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wametangaza upande mmoja makubaliano ya kusitisha mapigano leo Jumapili, ili kujaribu kupunguza mgogoro wa kibinadamu magharibi mwa taifa hilo.
Mashambulio dhidi ya jeshi la taifa hilo yanayotekelezwa wapiganaji wa Arakan Rohingya Salvation Army, yalisababisha mapigano makali ya wiki mbili, ambapo zaidi ya watu laki tatu wa jamii ndogo ya Warohingya wamekimbilia nchi jirani la Bangladesh.

Kundi hilo la waasi, yameiomba jeshi la nchi hiyo pia kuitisha wito wa kusitisha mapigano, huku likiomba mashirika ya utoaaji misaada ya kibinadamu kurejelea kazi zao za kusambaza misaada.
Waziri mmoja wa serikali ya Myanmar ameiambia BBC kuwa, wengi wa Wa-Rohingya waliokimbia nchi hiyo na kuelekea Bangladesh, hawataruhusiwa kamwe kurejea Myanmar.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad