Watumishi Mkoani Geita Wakamatwa kwa Kuiba Dawa za Serikali

Watumishi Mkoani Geita Wakamatwa kwa Kuiba Dawa za Serikali
WATUMISHI wawili wa zahanati ya Kata ya Kakubilo wilaya na mkoa wa Geita wamekamatwa na wananchi wakidaiwa kuiba dawa  za  serikali na vifaa tiba na kuficha kwenye makazi yao kwa lengo la kupelewka kwenye maduka binafsi ya dawa.

Mkuu wa Wilaya ya Geita,  Herman  Kapufi, akithibitisha kukamatwa  kwa  watumishi wa sekta ya afya wa zahanati hiyo, aliwataja kwa majina kuwa ni Peter Matono, mtunza  stoo ya dawa na mhudumu Enock Ngidangida na kusema walikamatwa na wananchi wakiwa wameficha dawa na vifaa tiba zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni saba kwenye makazi yao.

Kapufi alisema kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria madaktari na wahudumu wa afya watakaobainika kujihusisha na tabia hiyo.

Alisema watuhumiwa hao kwa sasa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani hapa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad