Wazili wa Elimu Nchini Kenya Amesema Moto Uliowaua wanafunzi 9 wa Shule Ulianzishwa Makusudi

Wazili wa Elimu Nchini Kenya Amesema Moto Uliowaua wanafunzi 9 wa Shule Ulianzishwa  Makusudi
Waziri wa elimu nchini Kenya Fred Matiang'i amewaambia waandishi wa habari kuwa moto amboa ulitokea katika shule moja ya bweni kwenye mji mkuu Nairobi mwishoni mwa wiki, ambapo wanafunzi 9 walifariki ulianzishwa makusudi.

"Moto huo haukuwa ajali bali ulianzishwa makusudi", alisema Matiang'i.
Ripoti za vyombo vya habari zilisema kuwa takriban wasichana 10 wa shule ya wasichana ya Moi bado wamelazwa hospitalini.
Awali Matiang'i alisema kuwa shule hiyo itafungwa kwa wiki mbili huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na sababu ya moto huo.
Hata hivyo alisema kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajianda kufanya mtihani wa kidato cha nne wa KCSE.

Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo, mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliotibiwa baada ya kisa hicho alisema kuwa moto huo ulianza mwendo wa saa saba usiku.
Watoto 20 wafariki katika ajali Afrika Kusini
Alisema kuwa bweni lililochomeka lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu kujinusuru.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad