Waziri Mwijage aAkiri Kukwamishwa na Baadhi ya Taasisi Serikalini


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amelalamikia baadhi ya taasisi za serikali kumkwamisha kwenye utekelezaji wake kwa kuchelewesha kutoa vibali kwa wawekezaji.

Mwijage amesema hayo kwenye uzinduzi wa Bodi mpya ya TIC jana jijini Dar es salaam huku akiitaka bodi hiyo kuchukua jukumu hilo la kuwaambia ukweli taasisi za serikali zinazokwamisha uwekezaji nchini kwa kuchelewa kutoa kibali na kusema kuwa watambue mchezo wao huo ni mauti kwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

“TIC nategemea mtakuwa na jukumu la kuziambia taasisi za zingine za serikali kwamba hamfanyi vizuri na kwamba mchezo wenu ni mauti kwetu, kama mimi natafuta wawekezaji nasafiri, nabembeleza, nasalimia watu ambao wasingepata nafasi ya kusalimiana na mimi, nakosa kukaa na familia yangu, nakosa kukaa kwenye jimbo langu, nasafiri nazunguka naleta wawekezaji halafu yupo mtu anatumia mwezi mzima au miaka miwili kutoa kibali, TIC mnapaswa mniambie” amesema Waziri Mwijage kwenye uzinduzi wa bodi mpya ya TIC.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),  Bwana Godfrey Simbeye ametahadharisha wanasiasa kuhusu kauli zao zinazowakatisha tamaa wawekezaji kuacha mara moja.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad