Wema Sepetu Full Kicheko Baada ya Manji Kuachiwa Huru

Baada ya mfanyabiashara mashuhuri nchini, Yusuf Manji kuachiwa huru na Mahakama ya Kisutu jijini Dar, Staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu ameonyesha kufurahishwa na kitendo hicho kutokana na ujumbe aliouandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Siku za nyuma Wema alikuwa akiposti picha za Manji na kuandika ujumbe wa kusikitishwa na kumuonea huruma mfanyabiashara huyo, lakini saa chache baada ya kusambaa kwa taarifa za kuachiwa, ameposti tena picha ya Manji na kuandika maneno yafuatayo:

“Alhamdullilah”

Manji ameachiwa huru leo Septemba 14, baada ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kuiambia mahakama kuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nakupenda Wema
    sauti yako ni ya pekee

    ReplyDelete
  2. nice its was good for manji kutoka kwani kuna mtu bado ana dukuduku aaaah

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad