Naibu Waziri wa Afya, Hamisi Kigwangalla amefunguka na kusema haagizwi na kila mtu kwa kuwa ni kiongozi bali wenye mamlaka ya kufanya hivyo ni wananchi wake wa Nzega vijijini pamoja na maagizo anayoyapata kutoka Rais wa nchi.
Mh. Kigwangalla ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo watu mbalimbali wamekuwa na mawazo tofauti tangu alipohoji suala la ajira nchini na baadhi ya watu kumuagiza kwa Mh. Rais kufikisha ujumbe kuhusu hali ilivyo mitaani haswa kwa vijana.
Kutokana na ombi hilo Mh Kigwangala alijibu kwa mtindo wa swali na kusema, "Mnanitukana halafu mnanituma? Wenye mamlaka ya kuniagiza ni wananchi wa Nzega Vijijini tu kwa upande mmoja, na Rais kwa upande wa pili! wengine No" Dkt. Kigwangalla.
Pamoja na jibu hilo wapo ambao walihoji uongozi wake wa kuwatumikia viongozi wa Nzega wakati yeye ni Naibu Waziri wa Tanzania
"Yes...natumikia sekta tano za Wizara kwa maelekezo na maagizo ya Rais tu basi! Ambayo yapo kwenye dhamana aliyonipa, siagizwi na kila mtu" Kigwangalla
Kupitia ukurasa wake huo ambao umechangamka tangu wiki iliyopita alipoweka maoni yake juu ya usaili wa awamu ya kwanza kwa wanaotafuta ajira katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) uliyofanyika Agosti 30, 2017 na kuuliza kwamba kama picha hiyo inaashiria ukubwa wa tatizo la ajira nchini au watu wanachagua sana kazi za kwenda jambo ambalo liliibua mijadala mingi ambapo wengine wakihoji kwa nini yeye kakubali kuajiriwa.
Baadhi ya jumbe ambazo zipo kwenye ukurasa wa Mh. Kigwangala zenye maoni tofauti
Aidha pamoja na majibu ya kiongozi huyo hususani kuwataka vijana wajiajiri wapo ambao wamemtaka yeye kama angeonyesha mfano kwa kukataa nafasi ambayo amepewa na Rais Magufuli ili watu waamini kwamba ni muumini wa kujiajiri.
Pamoja na swali hilo kutoka kwa wachangia hoja, Mh. Kigwangalla alijibu "Ulitegemea nikatae kuitumikia nchi yangu. Ulitegemea nitumwe kazi na Rais wa nchi yangu nikatae? Uzalendo wa wapi huo. Nidhamu ya wapi hiyo?
Wenye Mamlaka ya Kuniagiza ni Wananchi wa Nzega Pamoja na Rais Ila Siagizwi na Kila Mtu
0
September 04, 2017
Tags