Wilaya ya Temeke, Ilala Kinara wa Unyanyasaji wa Kijinsia

Wilaya ya Temeke, Ilala Kinara wa Unyanyasaji wa Kijinsia
Wilaya za Temeke na Ilala zimetajwa kuwa na matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za utotoni na kukithiri kwa vitendo vya ukeketaji, huku Kata ya Kitunda wilayani Ilala ikiongoza kwa kuwa na kiwango cha juu cha matukio yaliyoripotiwa.

Akizungumza leo Jumanne kwenye mkutano wa mrejesho wa mradi wa kuhamasisha jamii kutokomeza ndoa za utotoni, ukeketaji na mimba za utotoni, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto(CDF), Koshuma Mtengeti amesema mradi huo ulilenga kuelimisha jamii juu ya madhara ya vitendo hivyo.

"Vitendo hivi vingi vimekuwa vikiripotiwa zaidi wilaya za Temeke na Ilala kwa mkoa wetu wa Dar es Salaam, hivyo CDF tukaamua kupeleka mradi wetu Kitunda ambako namba ya waathirika ulikuwa kubwa zaidi," amesema Mtengeti.Mkurugenzi Mtendaji wa CDF, Koshuma Mtengeti

Mkurugenzi Mtendaji wa CDF, Koshuma Mtengeti akizungumza katika mkutano wa mrejesho wa mradi wa kuhamasisha jamii kutokomeza ndoa za utotoni, ukeketaji na mimba za utotoni. Picha na Herieth Makwetta.

Amesema lengo ulikuwa kuondoa mila potofu kama ukeketaji pamoja na kutafuta ufumbuzi kwa pamoja wa jinsi gani jamii itashiriki katika kuwalinda watoto wa kike na kuhakikisha jamii inakuwa mstari wa mbele katika kutokomeza vitendo hivyo.

"Vitendo hivi vinawaathiri watoto wa kike hivyo tulilenga kuhakikisha kwamba  wanatambua haki zao na kuzitetea."

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Watoto na Ustawi wa Jamii Ilala, Joyce Maketa amesema jukumu la kumlinda mtoto ni la mzazi, mwalimu na mlezi na si mtu mwingine.

Ametoa rai kwa jamii kabla kumhukumu mtoto kuangalia mzizi wa tatizo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad