Wiliam Ngeleja Ajisalimisha Polisi na Kuhojiwa Kwa Lisaa Limoja Baada ya Ripoti ya Almasi na Tanzanite Kumtaja

Wiliam Ngeleja Ajisalimisha Polisi na Kuhojiwa Kwa Lisaa Limoja Baada ya Ripoti ya Almasi na Tanzanite Kumtaja
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amehojiwa kwa saa moja katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Septemba 11.

Ngeleja ambaye pia amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini wa awamu ya nne, aliwasili katika ofisi hiyo saa nne asubuhi akiwa peke yake ambapo alikutana na DCI saa tano na kuondoka saa sita na nusu mchana bila kusema alichohojiwa.

Hatua ya Ngeleja kufika ofisini hapo ni kuitikia wito wa Mkuu wa Jeshi La Polisi (IGP), Simon Sirro ambaye aliwataka watuhumiwa waliotajwa katika ripoti ya Tanzanite na Almasi kuripoti kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya mahojiano wakati uchunguzi ukiendelea
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad