Yaliyojiri Uwasilishaji wa Ripoti ya Makinikia ya Almasi na Biashara ya Tanzanite. Mruma, Maswi na Muhongo washutumiwa


Aliyewasirisha Ripoti hiyo ni mbunge wa Ilala, Musa Azan Zungu na anaongelea kamati iliyoyabaini ikiwemo kutowajika kwa mamlaka zinazohusika na almasi na Tanzanite ikiwemo NEMC na wizara ya nishati na madini.

Kamati ilibaini kutolipwa kwa income tax ikiwa kinyume na kifungu cha kodi kinacholazimisha kampuni za madini kulipa kodi. Kampuni ya Williamson haijalipa income tax kutoka 2007 mpaka 2017 kwa kisingizio cha kupata hasara.

Mapato stahiki nchi inatakiwa kupata ni kodi kwani mrahaba ni kiasi kidogo ambacho huwa ni fidia. Kuna mkanganyiko wa takwimu kwenye mauzo ya almasi. Kuna takwimu zinazokinzana ambapo nishati na madini na wakala wa madini(TIMA) umebaini kutofautiana kwa takwimu kutoka taasisi hizo mbili za serikali.




  • Kamati imebaini kwenye vyumba ambavyo Almasi huwa inahifadhiwa, kuna milango ya dharura ambayo hutumiwa vibaya.
  • Serikali inapata hasara kubwa kutokana na usafishaji wa Almasi nje ya nchi ambao hudaiwa kuwa inapungua thamani.
  • Kamati imeona kuna haja usafishaji wa mwisho wa madini ya Almasi ufanyike hapa nchini kwani haihitaji uwekezaji mkubwa.
  • Kutokana na kukosa mapato stahiki, kuna haja ya Serikali kupitia misamaha yote ya kodi ya madini ya Almasi hapa nchini.

Thamani ya Madini ya Almasi yanayouzwa nje ya nchi ni kubwa zaidi ukilinganisha na kodi inayolipwa hapa nchini.

  • Kwa maoni ya kamati kwa uamuzi wa serikali kutoinunua Petra kwa dola milioni 10 umesababisha hasara kwa sababu kwa sababu mgodi umezalisha almasi zenye thamani ya dola milioni 343. De Beers waliuza hisa bila kufata utaratibu, kamati ikiongozwa na waziri wa wakati huo, Ngonyani walitoa ushauri usinunuliwe.
  • Viongozi wa serikali waliopendekeza mgodi usinunuliwe ndio waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bodi.
  • Kamati ilipowahoji wajumbe wa bodi, Professa Jairo na Prof Mruma chini ya kiapo, Prof Mruma aliiambia kamati alishindwa kufuatilia madeni(Akiwa mwenyekiti wa audit commitee ya mgodi) kwa sababu hakuwa na muda wa kusoma na aliawaamini waliompelekea taarifa hizo baada ya kamati kumuhoji madeni yaliyobambikwa kwa serikali yamekuwa ni mengi mno.



  • Kamati ilimuhoji mheshimiwa Maswi ambae alikuwa katibu mkuu na ni mmoja alietia saini mkataba ambao kamati inaona una utata, alijibu hata yeye aliona kilichofanyika ni upuuzi mtupu na alienda mara moja Tanzanite one na alichukia na kutorudi tena ilhali akiwa ndie msimamizi wa wizara.



  • Kamati imebaini kuna zawadi ilitolewa kwa kiongozi mmoja mkubwa, zawadi hio ya almasi kwa sasa inakadiriwa kuwa na thamani ya dola milioni 200.
  • Makinikia yaliyobakiwa yanakadiriwa kuwa na thamani inayokadiriwa kuwa trilioni 2.3. Kamati inahoji mbona taarifa haikutolewa na yalichimbwa na marehemu Wilamson miaka ya 50? Wataalam wahakikishe gharama za makinikia hayo hazijumuishwi kwenye gharama za mgodi.

Inasikitisha kuona watumishi wa serikali hawajui kinachoendelea kwenye makampuni ambayo walipaswa kuyasimamia.

Zungu amempongeza Rais Magufuli kwa kuliamsha dude na wao wanaendelea nalo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu zangu, na wananchi wote kwa ujumla. Hii iniaumiza Roho zetu na Kuleta Huzuni katika Mioyo yetu.
    Inaleta fikira za kuangalia uongozi wote uliopita toka tulipo pata Uhuru mpaka leo.
    Na Dosari ni dhahiri zimeanzia kwa Mbamba Bey... Lakini Mungu kazipokea Dua Zetu na kujibu maombi ya Sala Zetu.
    Leo Amekuja Magufuli na Nia Njema na Uchungu wa kuiona nchi yetu na watu wake kuwa Duni.
    Haiwezekani kwa watendaji tuliowaamini kufanya khiyana Dhidi ya Taifa na Majukumu tuliowapa kuyatekeleza na wakajali UBINAFSI.
    Yunajiuliza je kwa sasa hatua gani tuichukue Dhidi yao na Kurekebisha Mishahara na Kusubsidize essential commodities and services ili watu waweze kuyamudu maisha na kuwa na Roho ya kutosheka badala ya TAMMAAA.
    Tukumbuke sisi wote kila mmoja wetu anapaswa kuwa MUADILIFU KATIKA NAFASI YETU ALIYOPEWA KIUTENDAJI NA TUMUOGOPE MUNGU KUNA SIKU TUTAULIZWA NA MALIPO YATATOKEA HAPA HAPA DUNIANI.
    TUPENDANE NA TUWE WAZALENDO KATIKA NYOYO ZETU.
    LEO TANZANIA SI NCHI YA KUWA HAPA ILIPO.
    TUMUOMBE MUNGU MAGUFULI NA TUMPE USHIRIKIANO UNASTAHIKI KATIKA KURUDISHA TAIFA LETU MAHALI PAKE.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad