Yanga, Ndanda FC Kuonyeshana Ubabe Leo Uwanja wa Uhuru

Yanga, Ndanda FC Kuonyeshana Ubabe Leo Uwanja wa Uhuru
Timu ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inatarajiwa kushuka dimba la uhuru leo Jijini Dar es Salaam kuwavaa Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu mzunguko wa nne huku wakiendelea kumkosa mshambuliaji wake Amisi Tambwe.

Hayo yamewekwa wazi na Kocha msaidizi wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa na kusema Tambwe ndiyo mchezaji pekee atakaendelea kuukosa mchezo huo wa leo.

"Kwa ujumla kikosi chetu kipo vizuri kabisa kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Ndanda FC", amesema Nsajigwa.

Amisi Tambwe amekuwa yupo nje (benchi) tokea ulipoanza msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na maumivu ya goti ambayo yalimuanza msimu uliopita.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad