Zitto Kabwe Amjia Juu Spika Job Ndugai....Adai Anawaangusha Wabunge

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kuwa anamsikitika sana kama haoni jeshi heshima ya Bunge inavyoshuka.

Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge Zitto Kabwe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni.

Kufuatia wito huo Zitto Kabwe amesema yeye atafika kwenye kamati hiyo ya maadili na Madaraka ya Bunge kama ambavyo Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza na kusema kuwa spika huyo kama angeweza kujua nguvu yake wala asingehaika na wabunge ambao wanakosoa kwa staha.

"Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili, Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu kushuhudia mbunge anapigwa risasi mkutano wa bunge ukiendelea wabunge wazoefu tulikuwa na matumaini makubwa na spika Ndugai tulimpigania dhidi ya njama za kumhujumu kutoka Ikulu anatuangusha angejua nguvu aliyonayo kukabili udikteta unaonyemelea nchi yetu asingehangaika na ukosoaji wenye staha tunaoufanya" alisema Zitto Kabwe

Aidha Zitto Kabwe amesema kuwa Ndugai alitamani kufikia japo robo marehemu Sitta katika kuongoza shughuli za bunge lakini ameshindwa kufikia hata asilimia ya Anna Makinda.

"Kwenye mazishi ya Spika wa watu Mzee Sitta, Ndugai aliomba afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda miaka 2 sasa hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa na Rais kwamba aliuliza wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge" alisema Zitto Kabwe
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Si makosa kutafuta haki za nchi na binadamu kupitia mataifa ya nje. Kusema si kutenda. Ni mbinu kila nchi hasa nchi kuu kama Marekani zinafanya hivi ili kudai haki, kuleta Amani. Hili si kosa la jinai. Watanzania wengi sana na serikali zetu, hatujui namna gani kimataifa tushirikiane, kutetea haki . Mpaka watu muuelimike hasa ndipo mtalielewa. Na kuchukua nguvu mkononi kumuua mtu bila kujua sheria matokeo ni haya. Huna ruksa ya kutoa uhai wa mtu kama kuku bali ni Mungu. Tutakapoweza kujielimisha na kuuthamini uhai wa kila Mtanzania ndipo tutaweza kuzungumza. Kwa sasa ni mashabiki na webgi wasio na elimu hawawezi kutofautisha mambo. Umafia si suhishi, bali elimu bora, sheria zifuatwa kiuongozi, na Katiba ituamulie mambo si akili za mtu mmoja au uoga wa mtu mmoja. Hatutakuwa na amani hata.Nchi lazima iendeshwe kwa misingi bora.Kuna haja kubwa ya kutoa elimu kwa Watanzania wote hasa vijana ili wajue haki zao na sheria zote za nchi. Nchi ipo mrama.

    ReplyDelete
  2. Mie sijakielewa wewe zito. Unataka nini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad