Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imefunguka na kusema kuwa haina uwezo wa kulipa dollar milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.
Akiongea leo Oktoba 20, 2017 kwa njia ya simu na chombo cha habari cha Kimataifa cha Uingereza (Reuters) Afisa wa Fedha wa Acacia, Andrew Wray kampuni hiyo haina uwezo wa kulipa fedha hizo kwa serikali ya Tanzania.
Washirika wakubwa wa Acacia, Barrick Gold siku ya jana Oktoba 19 walikubalina na serikali ya Tanzania kuwa watalipa dollar milioni 300 kwa serikali ya Tanzania pamoja na kugawana mapato yanayotokana na shughuli za uchimbaji wa madini nchini.
Chanzo cha habari tovuti ya Reuters.
ila Ina uwezo wa kuwaibia wafrica?
ReplyDeleteBoss wao Barrick ameshasign kuwa watalipa. Ikiwa Acacia hawana pesa waende wakakope bank wasilete ujinga
ReplyDeleteSasa huyu lidudu mtu anatingisha kibiliti. Ni kawaida huyu ndio nani godono blaun
ReplyDeleteAndru will be fired.
ReplyDeleteHe was not Authorised to communicate. On issues pertaining to the trached agreement