Acha Yanga Washangilie Suluhu,Simba Wanahitaji Mchumi Kuliko Manara

Na Thadei Ole Mushi.

Simba wanashangaa kwa nini Yanga wanashangilia kutoa Sare na Simba. Waacheni washangilie kwa nguvu zote. Hii ni match ya tatu msimu huu Yanga wanatoa sare na Simba katika dakika 90 za mchezo achana na match zilizoamuliwa kwa mikwaju ya penalt.

Simba Vs Yanga kwenye mapinduzi CUP walitoka sare ndani ya dk 90. Simba vs Yanga kwenye ngao ya hisani walitoka Sare ndani ya dakika 90. Simba vs Yanga kwenye match ya raund ya kwanza msimu wa 2017/2018 nayo wametoka sare.

Hapa ndipo napoona umuhimu wa kuwa na mchumi mwenye uelewa mkubwa pale Simba kuliko Haji Manara mpiga domo na mwenye mpira wa propaganda.

Kwa wale waliosoma course za uchumi na biashara watakuwa wanafahamu kitu kinachoitwa “Value for Money”. Ni kipengele kinacho deal na kuangalia thamani ya pesa iliyotumika kununulia bidhaa flan. Hapa tunafanya ulinganisho wa fedha zilizotumika na bidhaa iliyonunuliwa au huduma iliyonunuliwa.

Kwenye value for money tunaangalia pia effectiveness na efficiency kwamba je huduma au bidhaa hii niliyowekeza ina uwezo wa kufanya kazi kwa kiwango gani? Je input tulizoweka zinatuletea output tarajiwa?

NINI NAMAANISHA?

Nimeaangalia uwekezaji wa Simba kwa msimu huu kwa Mujibu wa taarifa zao wanadai walisajili kwa kiasi cha shilingi Bilion 1.3. Simba inaweza kuwa ndio timu pekee iliyosajili kwa Dau kubwa kuliko club zote za Afrika mashariki.

Nimeangalia kambi waliyoweka Simba kujiandaa na msimu huu, walienda South Africa kwa takribani mwezi mmoja. Walienda timu nzima usafiri wa ndege kwenda na kurudi na huduma zote walizopatiwa south Africa kwa kadirio la chini kwa timu kama simba ni bilioni 1.5.

Nimeangalia kambi ya Simba katika kujiandaa na match za yanga ni za kiwango cha juu. Huwezi kulinganisha Kambi za simba na za yanga wanaochamgisha mashabiki ili wapate kula yao. Match ya jana Haji Manara anatuambia kuwa walilala Hotel ya Nyota tano Serena Hotel kikosi kzima hapa ni mamilioni ya shilingi yalitumika.

Nimeangalia mishahara ya wachezaji wa Simba jumla ya mishahara ya wachezaji wote ni milioni 100.4. Mfano Haruna Mwenyewe anakunja milioni 8.7 pale Simba kazidiwa Laki 3 na Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania anayelipwa shilingi milioni 9. Kwa kiwango hiki Haruna anaenda kuzurura na kubutua tu uwanjani.

Hamjanielewa tu kwa nini nalazimisha Simba wawe na mchumi anayeweza kuzipangia fedha za Simba matumizi sahihi ili zilete matokeo tarajiwa?

Mnajua Pius Buswita analipwa shilingi ngapi pale Yanga? Ni chini ya Nusu mshahara wa Niyonzima halafu bado anamfunika uwanjani. Mnajua shilingi ngapi analipwa Pato Ngonyani?

 Kelele za Haji Manara hazitaweza kuwafanya Simba kuchukua Ubingwa mwaka huu. Simba kwa uwekezaji wake walitakiwa kuwa na tofauti ya point kumi na timu nyingine si utofauti wa magoli.

Simba isitegemee kuwa mwaka huu watachukua ubingwa kwa kuwa na idadi kubwa ya magoli. Ni mara chache sana Bingwa huamuliwa kwa tofauti ya Magoli. Inaweza kupita misimu 4 ndio mkapata msimu unaoamuliwa kwa tofauti ya magoli.

NINI NAKIONA MBELE.

Simba ilianza ligi kwa kishindo kikubwa ila imeaanza kuchoka. Ni tofauti na wenzao Yanga walianza Ligi wakiwa wamechoka sasa wanaanza kuimarika.

Kama Trend itaendelea hivi bingwa atakuwa Yanga. Hili halina ubishi…..

Acheni Yanga washangilie jamani fedha yao ni ndogo ila inafanya kazi kubwa sana. Nafikiri mnaona Brevis aliyopewa Ajibu inavyofanya kazi ya kuwalaza kina Mwanjale na viatu.

Acheni washangilie watu wanatokea Lodge za Kihonda Morogoro wanakuja kuwasumbua watu waliolala kwenye Hotel ya Nyota tano…..

Tuangalie Value for Money tuachane na Kelele za Manara.Simba iamue kufanya Biashara ya mpira kwa kutumia Fedha zao kwa usahihi.

Simba ijitafakari.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha ushabiki linganisha kwa haki. Weka na payrol ya yanga nayo uweke na usajili wao umetumia sh ngap kwa miaka hii miwil. Siwaelewag mnaojiita unaangalia upande mmoja. Weka na za yanga na azam na singida au haya timu ndogo. Kwanza si hakikuweka mishahar ya watu hadharan

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad