APR Bingwa Mashindano ya Nyerere Cup

APR ya Rwanda imetwaa mataji mawili ya mashindano ya mpira wa wavu ya Nyerere Cup 2017  baada ya kuifunga Jeshi Stars kwenye mchezo wa fainali ya wanaume na wanawake.

Mashindano hayo  yalianzishwa miaka 15 iliyopita  kwa lengo la kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere yalianza kutimua vumbi Oktoba 10 huku yakishirikisha jumla ya timu 13 kwa wanaume na 6 wanawake.

APR imeonyesha kuwa hawakuja kutembea baada ya kushinda michezo yote miwili ya fainali ya wanaume na wanawake kwa seti 3-0, 3-0 dhidi ya Jeshi Stars.

APR   Bingwa Mashindano ya Nyerere Cup
Kocha APR, Nkuranga Alexis amesema kuwa japo mashindano yalikuwa na ushindani, lakini wamepata walichotaka na haikuwa bahati kwao kushinda mataji hayo.

"Tulipoanza safari ya kuja Tanzania tuliweka malengo ya kufanya vizuri kwa kutwaa mataji ndicho kilichotokea, Tanzania inatimu nzuri ambazo zinaweza kushindana." alisema kocha huyo.

Kocha wa Jeshi Stars, Lameck Mashindano alisema kuna haja ya timu za Kitanzania kushiriki mashindano mengi ya kimataifa ili kujijenga zaidi kiushindani.

"Tumeshindwa kutetea taji lakini ndiyo michezo ilivyo ukikosa leo unaweza kupata kesho, mashindano ya kimataifa yatazijenga timu zetu, APR ilikuwa bora na ubora wao umechangiwa na kushiriki kwao mashindano mengi ya kimataifa." anasema kocha huyo.

Nahodha wa APR, Mwizere Ezic amedai siri ya wao kufanya vizuri kwenye mashindano hayo ni uzoefu ambao wamekuwa nao wa kushiriki mashindano mengi ya kimataifa.

Wanaume walianza kucheza kwa mfumo wa makundi matatu, kundi A lilikuwa na  APR  (Rwanda), Nyuki (Zanzibar),Chui, Mjimwema na Makongo (Dar es Salaam),kundi B  Jeshi Stars , JKT (Dar es Salaam), Police (Zanzibar) na Kigoma (Kigoma).

Kundi C;  Magereza ‘Tz Prisons’ (Dar es Salaam),Shinyanga  (Shinyanga) , Pentagon na Flowers (Arusha) na kwa upande wa wanawake wenyewe  wliocheza kwa mfumo wa Ligi kulikuwa na APR (Rwanda), Makongo, Magereza, Jeshi Stars, Mjimwema na JKT (Dar es Salaam).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad