Bunge Kuanzisha Uchunguzi wa Ufisadi Mkubwa Afrika Kusini

Bunge Kuanzisha Uchunguzi wa Ufisadi Mkubwa Afrika Kusini
Bunge la Afrika leo linaanzisha uchunguzi unaohusu madai ya ufisadi wa kiwango cha juu zaidi serikalini.
Wale waliopiga ramli kuhusu ufisadi huo na maafisa mashuhuri wanatarajiwa kuitwa kutoa ushahidi wao.

Muda huu huenda ukawa wa kukosa amani miongoni mwa watu wenye ushawishi nchini Afrika Kusini.
Mawaziri, watu matajiri, mtoto wa rais na mashahidi wengine wengi, wanatarajiwa kuitwa mbele ya wabunge wanaochunguza madai ya ufisadi mkubwa nchini humo.

Inadaiwa kuwa familia moja yenye nguvu ya Gupta, imekuwa na ushawishi wa viwango vya juu serikalini, ili kuweza kujishindia kandarasi za serikali.

Familia hiyo ya Gupta imekana madai hayo sawa na rafiki wao Rais Jacob Zuma
Katika kipindi hiki cha misukosuko ya siasa kuhusu ni nani atakaye mrithi Zuma, uchunguzi wa wiki hii huenda ukawa na athari za aina yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad