Chadema Yakomaa Yasema Kama Chama Pinzani Wataendelea Kukosoa

Chadema Yakomaa Yasema  Kama Chama Pinzani Wataendelea Kukosoa
Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) kimesema kuwa kama chama kikuu cha upinzani wana wajibu wa kuwazungumzia wananchi na kukosoa Serikali.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zanzibar, Salum Mwalimu amesema hayo leo Jumatano wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Kumekuwapo na juhudi nyingi za kutuzima midomo, hatutakubali mitutu wala nini, tumezaliwa siku moja tutakufa siku moja,” amesema Mwalimu.

“Tutasema, tutakosoa na kukemea na hatutakubali kurudi nyuma hata siku moja na tunawahakikishia Watanzania hatutarudi nyuma,”

“Wako waliodhani matukio haya yataturudisha nyuma, hakuna jambo jema kama mshindani wako anapokuwa hoi na kweli wako hoi,” amesema Mwalimu.

Amesema mwaka jana walizungumza kuhusu Ukuta, kueleza kile walichokiona ambacho kinakuja siku za usoni na ndicho kinachotokea

“Tuliwaambia Watanzania harufu hii ya kutokuheshimu Katiba, sheria na ilianza kwa kuzuia mikutano, kamata weka ndani saa 48 wakasema si wanasiasa na tukawaambia ukiukwaji huu wa kisheria hautaishia kwa wanasiasa na ndicho kinaonekana,” amesema Mwalimu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad