Chadema Yapata Pigo Lingine
0
October 11, 2017
Chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa kimeendelea kujiimarisha kwa kuvuna wanachama watano kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa wakiwa na mikakati ya kuja kulikomboa jimbo la Iringa mjini ambalo lipo chini ya chama cha CHADEMA.
Akizungumza wakati wa kuwapokea wanachama hao kutoka kata ya kitwiru mwenyekiti wa CCM manispaa ya Iringa Said Rubeya aliwapongeza wanachama kwa kutambua kazi inayofanywa na chama cha mapinduzi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano DR John Pombe Magufuli.
“Mimi nimefurahi sana nyie kurudi nyumbani maana mtakuwa na msaada mkubwa sana katika kukijenga chama hapa manispaa ya Iringa ili tuweze kulikomboa jimbo hili katika uchaguzi ujao na hii ndio mikakati yetu” alisema Rubeya.
Rubeya aliwaambia wanachama hao kuwa sasa wapo katika mikono salama ya kisiasa tofauti na walipokuwa kwenye chama cha awali na kuwasihi wasiwe waoga katika kufanya kazi za kukijenga chama cha mapinduzi.
“CCM ndio chama tawala hivyo ondoeni hofu na mzidi kutupa maarifa mliyotoka nayo huko na kukisaidia chama hiki kuzidi kupata wananchama wengi kutoka vyama vya upinzani na mkiwa CCM mtapikwa vizuri na kuwa viongozi wazuri” alisema Rubeya.
Aidha Rubeya aliwaambia kuwa CCM hutoa madaraka kwa mtu yeyote yule mwenye weledi katika nafasi aliyogombea, hivyo huku hakuna kuteuana huku kuna nafasi za kugombea na kuchaguliwa na wanachama wa chama cha mapinduzi tofati na kule mlikokuwa mnateuna kwa maslai ya mtu mmoja.
Naye katibu wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Marko Mbaga aliwataja wanachama waliohamia chama hicho kutoka CHADEMA ni Baraka Kimata aliyekuwa katibu mwenezi na Diwani wa kata ya Kitwiru,Theodora Mbata aliyekuwa matroni wa wanawake kata ya Kitwiru, Erick Muyungo na Raymond kimata aliyekuwa kiongozi wa redbrigad manispaa ya Iringa na katibu mwenezi wa kata ya kitwiru.
“Hii ni mwanzo tu watakuja wengi mno kwa kuwa CCm manispaa ya Iringa wanachapa kazi hata kama halmashauri ipo kwa wapinzania lakini wao wataendelea kufanya kazi kwa kutekeleza ilani ya chama chetu ili kuwamaliza wapinzani wetu wote warudi kwenye chama tawala” alisema Mbaga
Edwin bashir ni katibu wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa alisema kuwa sasa ni wakati wa kufanya kazi kwa wananchi na wananchi waendelee kuwa na Imani na chama cha mapinduzi ili waje kufanikiwa kulikomboa hili jimbo ambao lipo upinzani.
“Mimi najua vijana wengi muda sio mrefu wataanza kurudi nyumbani kwao kwenye chama wananchokipenda na kuondokana na siasa za maji taka kwa kuwa CCM ni tanuli za kuwahoka viongozi bora na sasa manispaa tutafanya kazi kweli kweli na kuwamaliza wapinzani kwa nguvu zote” alisema Bashir.
Baraka Kimata,Theodora Mbata, Erick Muyungo na Raymond kimata walisema kuwa watakitumikia ipasavyo chama cha mapinduzi kama walivyokuwa wanakitumika chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhakikisha CCM wanashinda chaguzi zote watakazo kuwa wanashiriki katika manispaa ya iringa.
Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM Ritta Kabati aliwapongeza viongozi wote wapya waliochaguliwa hivi karibuni na kuanza kufanya kazi inayoonekana machoni mwa wakazi wa manispaa hiyo.
“Juzi mmechaguliwa lakini kazi imeanza kwa kuwapata wananchama wapya wanaotoka upinzani kurudi CCM hiyo sio kazi ndogo kwa kweli hiyo ni kazi kubwa sana ambayo mmeanza nao nichukue nafasi hii kuwapongeza kwa mnachokifanya kuhakikisha tunapata wanachama wengi kutoka upinzani” alisema Kabati.