Daktari: Tulifungua Ubongo wa Kanumba na Kuukuta Umevimba na Kisogo Kilikuwa na Mgando wa Damu

Daktari: Tulifungua Ubongo wa Kanumba na Kuukuta Umevimba na Kisogo Kilikuwa Mgando wa Damu
KESI inayomkabili muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’,  imeendelea kusikilizwa leo Jumatatu, Oktoba 23, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo shahidi wa nne upande wa Jamhuri anatoa ushahidi wake.
Katika ushahidi huo imeelezwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Binadamu  wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dtk. Innosent Mosha ambaye ni shahidi wa nne wa kesi hiyo, aliletewa oda  kutoka Jeshi la Polisi kwamba aufanyie uchunguzi mwili wa Steven Kanumba uliokuwa mochwari akishirikiana na daktari mwingine.
“Tulifungua ubongo wa Kanumba na kuukuta umevimba, mishipa midogomidogo ya ubongo ilikuwa imeingia damu, lakini kabla ya kufungua ubongo, kwenye kisogo kulikuwa na mgando wa damu.
“Baada ya kumaliza uchunguzi wetu tulipeleka sampuli kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo tulipeleka pia sampuli mbalimbali za viungo vya mwili wake,” amefafanua Dkt. Mosha.
Ushahidi bado unaendelea kutolewa mahakamani
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad