Dangote Aonya Sera za Uwekezaji za Magufuli...Adai Zinawaogopesha Wawekezaji

Tajiri namba moja barani Afrika Aliko Dangote ambaye pia ni mwekezaji mkubwa nchini Tanzania amemuonya Rais John Pombe Magufuli kuwa sera zake nchini humo zinawaogopesha wawekezaji.
Dangote ambaye amewekeza dola za kimarekani 650 kwenye uzalishaji wa saruji, amesema ni wakati umefika kwa raisi Magufuli kuzipitia upya sera zake ama akubali kuingia katika hatari ya kuwapoteza wawekezaji wote nchini humo.

Raisi Magufuli alipoingia madarakani, wawekezaji na wafanyabisahara walifurahishwa kwa jinsi alivyopambana na rushwa lakini miaka miwili baadae, baadhi ya wafanyabiashara wamegubikwa na hofu hasa baada ya kuona mazingira ya kibiashara yamebadilika kutokana na mfumo wake wa utawala.


Magufuli atoa agizo Dangote Group ipewe ardhi ya kuchimba mkaa wa mawe
Mapema mwaka huu rais Magufuli alianzisha uchunguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini uhalifu mkubwa ambao ulisababishwa kuundwa kwa sheria mpya ya madini.

Katika kongamano lililofanyika mjini London, mfanyabiashara huyo alisema sheria mpya zinazoundwa Tanzania zinaiweka nchi hiyo kwenye hatari ya kuwafukuza wawekezaji wote na kushindwa kuwarejesha tena.

Serikali nchini humo ina amini kwamba sheria hizo zitawanufaisha wananchi kutokana na rasilimali za taifa lao licha ya kwamba makampuni ya kigeni yamekuwa yakipinga mabadiliko hayo ya sheria kwa madai hazitekelezeki.

BBC Swahili
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sasa yeye Dangote anachukizwa na jitihada za serikali ya Magufuli kupigania wananchi wafaidike na rasilimali zao? Kama alitarajia kuja kuwekeza Tanzania ili iwe njia ya kujakujinifuaisha zaidi na rasilimali za Tanzania kwa kutumia kigezo cha udhaifu wa serikali na viongozi wa Africa katika masuala ya rushwa ataisoma namba. Hii ni Tanzania nyengine na Maghuful amekwisha sema tupo katika vita vigumu vilivyojaa fitna vita vya uchumi kwa hiyo mengi tutasikia. Dangote anjipambanua kuwa ni miongoni mwa maadui wetu katika vita takatifu vya uchumi kwa taifa letu. Kama alikuwa na nia ya kweli ya kutoa ushauri angewasiliana tu na serikali kutoa ushauri wake badala ya kwenda kupanua domo lake kwenye vyombo vya habari. If he think he can use his richness exploiting our economic weakness to do or say what ever he want then he is completely wrong and he will never ever suceed sowing what intending to do .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad