DC Kinondoni Atoa Siku Saba Wafanyakazi Walipwe Malimbikizo yao

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi ametoa siku saba kwa muwekezaji anaemiliki mgahawa wa Tangren uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa mgahawa huo wanalipwa stahiki zao za malimbikizo ya muda mrefu.

Akizuungumza jijini Dar es Salaam alipotembelea mgahawa huo DC Hapi  baada kupokea malalamiko kwa wafanyakazi wa mgahawa huo ambao wamedai kutolipwa malimbikizo yao kwa muda miaka kumi, na wamekuwa wakifanya kazi bila likizo wala ‘over time’, DC Hapi ameagiza stahiki zao zishughulikiwe ndani ya siku saba.

Pia DC Hapi ameagiza wafanyakazi hao waunganishwe kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii haraka iwezekanavyo na wapewe mafunzo ya namna inavyofanya kazi.

” Tunapenda sana wawekezaji lakini sio wawekezaji wasiofuata misingi na taratibu na sheria za nchi, namuomba muwekezaji huyu azingatie maagizo niliyotoa vinginevyo tutachukua hatua zaidi” Alsema DC Hapi.

DC Hapi ameeleza kuwa watafanya oparesheni ya kuwafutia leseni za biashara na kuwachukulia hatua wawekezaji wasiofuata sheria na taratibu za nchi, ambapo amesisitiza kuwa haitaji wafikie huko endapo watafuata sheria.

Katika hatua nyingine DC Hapi amewataka wafanyakazi kuwa na nidhamu ya kazi kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha kutoa visingizio visivyokuwa na sababu ya msingi kama walivyo lalamikiwa na mmiliki wa mgahawa huo Liu Deng Wei ambaye ameeleza kuwa wafanyakazi hao wamekuwa wakichelewa kufika kazini na kutoa visingizio visivyokuwa na msingi.

Pia DC Hapi katika ziara yake alitembelea kiwanda cha kutengeneza lifti cha SEC East African kilichopo Masaki na kuutaka uongozi wa kampuni hiyo kuweka mahusiano mazuri na wafanyakazi wao ili kutatua changamoto zinazowakabili.


DC Hapi amewashutumu vikali baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Kazi wanaoshirikiana na muwekezaji kuwanyonya watanzania wanyonge na kuhaidi atazifikisha taarifa kwa mamlaka ya juu wazifanyie kazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad