Diamond Afunguka Kuhusu Fedha Anazotumia Kufanya Kolabo na Wasanii wa Marekani

Diamond  Afunguka Kuhusu Fedha Anazotumia Kufanya Kolabo na Wasanii wa Marekani
Diamond amefunguka kuhusu fedha anazowalipa wasanii wa Marekani kwa ajili ya kufanya kolabo.

Akiongea na Dizzim Online hit maker huyo wa Hallelujah amesema kuwa hakuna fedha yoyote ambayo amewahi kumlipa msanii yoyote wa nchi hiyo ambao tayari ameshafanya nao kolabo.

“Mimi sijawahi kulipa kolabo yoyote kwanza ya Marekani niliyowahi kufanya, sijawahi kulipa na ukichunguza kiundani kolabo zangu na Wamarekani siyo kitu ambacho ‘nimejishobokesha’ ni watu wenyewe ambao wanatokea kunikubali na kuupenda muziki ambao ninaufanya,” amesema Diamond.

Msanii huyo ameongeza, “Ndio maana unaona sometimes sipost naona kama sina haja ya kupost ikiwa wao wenyewe wanakuwa wanafurahi na wanapenda kupost kitu tunachokifanya. Sometimes naogopa kupost naonekana kama nitajishauwa, sitaki kuonekana hivyo, nataka nionekane pointi yangu kuuchukua muziki wa Tanzania kuupeleka mbali.”
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. manfiki mkubwa kama Bi sanyula na Lemadolezz.

    ReplyDelete
  2. huna lolote la ukweli. una pesa ulizopata ukubwani ila akili huna. ops! unazo za kutoa kiki kwa kizee chako.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad