Alute Simon Mughwai, kaka wa Tundu Lissu ni wakili na ofisi yangu ipo Arusha.
Sababu za kuita hii press conferess ni kama zifuatazo;
- Kuwashukuru ninyi wanahabari kwa namna ambavyo mmendelea kutuhabarisha na kutoa habari kwa wananchi kwa umma juu ya maendeleo ya matibabu ya Mhe. Tundu
- Kwa niaba ya familia, naomba niweze kuwapa mrejesho juu ya hali ya Mhe. Tundu. Anaendelea vizuri ana imarika, amefanyiwa upasuaji mara kadhaa na sasa hivi yupo vizuri. Ameanza kula kwa njia ya kawaida na ameanza kuzungumza vizuri. Ndugu yetu ambaye ameenda kule mara ya mwisho juzi ameleta salamu kwamba yupo sawasawa na jana tumezungumza na mke wake
- Nilivyokwenda Nairobi tarehe 9, tulifanya kikao sisi wanafamilia, uongozi wa Chadema pamoja na uongozi wa chama cha wanasheria Tanganyika kwamba atakayekuwa natoa taarifa juu ya matibabu ya Tundu ni Mhe. Mbowe pekee. Yeye ndio atatoa taaarifa rasmi na wali si mwingine yeyote
Kama ambavyo wengi wenu ambavyo mtakuwa mmepata habari, sisi familia tuliandika barua serikalini kuomba kwamba kwenye jambo la uchunguzi la huo uovu ulikwisha fanywa, lifanyiwe upelelezi wa kina, wa haraka na wa kitaalam ili hao waovu wakamatwe na wapelekwe kwenye mikono ya sheria.
Kwenye kuifuatilia barua hiyo, tumeonana na Waziri wa sheria na mambo ya katiba jana na leo mchana huu tumetoka kuonana na mwanasheria mkuu wa serikali kufuatilia habari ya hiyo barua. Wametupokea vizuri na wanaishughulikia
Katika kufutilia swala hili na kufanikiwa, Sisi kama familia tunadhani hatuwezi ku-ignore serikali lazima tuende nao mpaka hapo tutakapoona kwa mfano hiyo njia imefungwa. Sisi kama familia tunataka jambo hili liende kwa utaratibu wa kawaida sheria ifuatwe bila kuingiza siasa. Siasa kama itakuja ije wakati bwana Tundu yupo barabarani anatembea
Katika barua ile tulikuwa tumependekeza serikali kupitia jeshi la polisi waweze kushirikisha wataalamu wengine wa uchunguzi kutoka nje
Katika gazeti moja nilisoma wakimnukuu Waziri wa mambo ya ndani Mwiguli, sijui kama walimnukuu sawasawa ila kama walimnukuu sawa alisema "Tanzania ni nchi huru, inajitegemea, na ina vyombo vyote vya upelelezi na kadhalika ambavyo hinahitajika kufanya kazi na haitaji input ya vyombo kutoka nje"
Kwa mujibu wa sheria na sheria tuliyoitaja kwenye barua hiyo ni sheria ya ushirikiano katika mambo ya jinai. Sisi kweli ni huru, lakini sisi(Tanzania) ni sehemu ya jumuiya ya kimataifa. Hivyo tunashirikiana na nchi nyingine
Nimeona kwenye gazeti la leo likimnukuu IGP akizungumzia habari za yule dereva wa Mhe. Tundu aliopo Nairobi kwamba arudi nchini ili aje ahojiwe. Nadhani ameripiwa sawasa, sasa sisi ushauri wetu ni kwamba kwa nini Polisi wasimfuate kule Nairobi amekaa kwa takribani wiki tatu.
Aliyefanya uhalifu hajakamatwa maana yake maisha ya huyo dereva si yatakuwa yapo hatarini kuna utaratibu wowote wa kuhakikisha juu ya usalama wake. Isije ikawa anavuka Namanga kuja nchini anakatishwa pale njiani.
Hatupo tayari jambo hili likafanywa siasa, halafu na Tundu wanamfanya mpira wa kona, sisi tutakuwa wapi sasa tutakuwa washika vibendera au namna gani. ' we are not interested'
Vicent Mughwai (Mhadhiri wa Chuo Kikuu) anaongea na kusema;
Nakumbuka Lissu alifanya press conferenss tarehe 18/8 akasema kuwa kuna watu wanamfuatilia kila aendapo akataja hata aina ya gari na plate namba za hilo gari na nakumbuk anilona clip ya video akimtaka IGP na mkuu wa mashataka ili wawaambie wale vijana wafanye kazi nyingine na waache kumfuatilia. Na hawa ndio ilikuwa wa kuanza nao
Sasa tunavyoambia mpaka leo hakuna aliyeshikwa pamoja na kwamba gari lilijulikana na plate namba ilitajwa. Nasikia waziri alisema hilo gari lipo Arusha na halijawahi kufika Dar, mimi nilipata kigugumizi kidogo kwa sababu hivi unajuaje halijawahi kufika Dar au mmelishika Arusha kumbe linajulikana ni la nani!
Kusema unasubiri mtu moja (dereva wa Lissu) zoezi limesimama, labda zoezi linaendelea lakini sisi kama familia tunaona hakuna seriousness wakati mtu alikuwa auwewe. Mtu ambaye amekuwa ma mchango mkubwa kwenye hii nchi.
Kwa msisitizo tu sasa zoezi hili haliendi itakiwavyo, labda kuna haja ya kushikisha wapelelezi toka nje. Kwasababu nia ni njema ya kutaka kujua aliyefanya hili tukio
Cha mwisho nitoe shukurani wa watanzania wote ambao kwa njia moja ama nyingine walikuwa wakimuombea Tundu kwa sala na kutoa michango mbalimbali.