Fastjet Yaleta Ndege Mpya Aina ya E190 Kukabiliana na ATCL Katika Soko la Ndani na nje ya Tanzania
0
October 05, 2017
Baada ya Air Tanzania kuibuka na ndege zake toka kampuni ya Canada,wao Fastjet wameibukia Brazil na kuleta ndege aina ya Embrer190 (E190),twin-jet engines.
Kuanzia juma lijalo,wateja wa Fastjet nje na ndani ya nchi wataanza kusafiri na ndege aina ya E190 ambazo ni "tamu" kwa usafiri wa ndani na nchi jirani(Mainlines and Regional Airlines).
Fastjet inatazamiwa kuongeza ndege mbili aina ya E190,ambazo kwa ujumla wake zitakuwa tatu pamoja na ile Airbus319 ambayo Fastjet imekuwa ikiitumia kwa miaka mitano sasa.Ujio wa E190 ni changamoto kubwa kwa Air Tanzania na DH8-Q400(Bombardier) ambazo mpaka sasa,AirTz wanazo mbili tu.
Kuna habari kuwa Fastjet,akiwa na hizo E190 ataanza kwenda kwenye "destinations" ambazo hapo awali zilikuwa zinatawaliwa na Air Tz
Kigoma,Mtwara,Mbeya,Arusha,KIA,Mwanza,Tabora,Zanzibar na nchi ya Commoro ni maeneo ambayo Fastjet anatazamiwa kwenda na kuleta ushindani mkubwa kwa shirika letu la Taifa(National Carrier)
Uzuri wa E190,ni jet engines,pia ina mwendo kasi na comfortability.Safari ya Dsm Mbeya ni dakika 35 mpaka 40,wakati ile ya Mwanza ni dakika 55,hali ambayo ni kinyume kabisa na "pangaboi" zetu za ATCL.
Jukumu la ATCL kwa sasa,ni kufanya juhudi ya "kuikomboa" hiyo bambadia moja iliyoshikiliwa,kuleta kwa haraka zile Bombardier CS300 ambazo ni "jet engines" tulizoambiwa zipo mbioni kuja ili kukabiliana na ushindani wa Fastjet.
Bila kupepesa,ujio wa E190 katika "route" ambazo ATCL anakwenda,tena katika ulimwengu wa soko huria,utaleta changamoto na ushindani mkubwa sana kwa shirika letu la ATCL.Ndege za E190 zina raha yake,hizi ndio ndege ambazo Kenya Airways anazitumia kwa safari zake za ndani ya Afrika kwa muda mrefu sasa.Ujio wake katika soko la usafiri wa anga Tanzania,ni ufunguo wa mapinduzi makubwa ya usafiri wa anga na changamoto mpya za kimaendeleo.
Juzi Rais ktk hotuba ya ALAT alisema "Tutaendelea kununua ndege nyingi mpaka shirika liimarike na Tanzania ipate maendeleo".
Ni matumaini yangu,ujio wa E190 za Fastjet,utaifanya Serikali iamke zaidi na kuimalisha shirika letu la ndege la ATCL.Tuondoke kwenye DH-Q400,tukimbilie haraka kwenye zile Bombardier CS300,kukabilana na hawa kasuku wa kijivu.
Barafu
Tags