Kwenye video ambayo anaonekana akizungumza, aliyekuwa diwani wa kata ya Kimandolu Mchungaji Rayson Ngowi, amesema kuna haja ya kutafuta hekima za Wilbroad Slaa, ili kukisaidia chama hicho kukaa kwenye mstari unaofaa, kwa kuwa sasa kimeanguka kwa kiasi kikubwa.
Bwana Ngowi amesema hata yeye kutoka CHADEMA ameondoka kwa kutaka mwenyewe na sio kununuliwa kama inavyodaiwa, na kwamba kuna wengine watakaofuata nyuma yao baada ya wao kuondoka kwenye chama hicho.
“CHADEMA ya leo sio ile ya Dkt Slaa, CHADEMA ya leo ni ya maslahi, CHADEMA ganganjaa, na wakikataa mimi nitasema, sikiliza Mbowe, chama chako kina matatizo makubwa, huna viongozi, kamtafute Dkt. Slaa nafikiri ataokoa jahazi, kama mnataka kurudisha imani, kwa sababu sio mimi tu nimeondoka watakuja wengi”, amesema diwani huyo.
Ye Slaa kama mzalendo na uchungu wa nchi hii atajua nini afanye. Kama alitaka uraisi tu atakaa huko na kujitokeza apendapo. Kama Mzaleno atarudi aungane nao. Na si wa kumbembeleza apate kichwa kikubwa kinachotawaliwa na mke wake. Atavimbishwa kichwa badala ya kuwa mtu wa watu. Chadema huu ni mpito tu. Ukweli wa nchi kielimu, kimaendeleo, kifikra unahitaji kiongozi zidi ya Magufuli. Amejitahidi anavyoweza, lakini hatayaweza yote kwa kuwa si msikivu, na kubana uhuru. Pia sijamwona akiwahukumu waliotufikisha hapa . Hajawataifishia mali zao. Bado anakula nao meza moja. Ingawa anajaribu kutumia Ilani za Wapinzani, hayupo serious kukomesha yote ambayo CCM wameyatenda na kutusababishia hasara. Bado anawaogopa Viongozi wa ngazi za juu ambao anawatetea. Angewachukulia adhabu hao na kuwataifishia mali zao, Tungekuwa na chance nzuri. Hawezi. Na hilo ndilo litakalomwangusha Raisi wetu. Ujasiri wa kuchukulia hatua madingi, au mapapa walioileta hii dhoruba. Huwezi kujenga ufa wakati mpasuko wa msingi umeoza. Atakapoamua kufanya hivi, hata hawa watoa rushwa wadogo wataufyata. Wanachukua rushwa wakijua ni adhabu ndogo tu, na watachukua mabilioni wakitakiwa kurudisha vijisenti. Hii haitalinyoosha Taifa kama loop wholes ni kubwa. Mwibaji elfu mbili kifungo miaka thelathini. Mwibaji mabilioni atakamatwa, achiliwa, kamatwa mwishoni yupo huru. Hili ndilo tatizo kubwa kwa ndugu Magufuli. Kuwahurumia waliomtangulia.Fyeka wote. Anza upya.
ReplyDelete