Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli halina jipya kwani sura zilizobaki ni zile zile.
Ameyasema kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter, ambapo amesema kuwa ameona mabadiliko ya baraza la Rais Magufuli lakini bado fikra ni zile zile na watu ni wale wale na kudai katiba mpya ndio suluhisho la vyote.
“Nimeona Mabadiliko ya baraza la JPM. Watu ni wale wale, fikra zile zile. Katiba Mpya yenye fikra mpya ndio tumaini kwa mabadiliko sahihi ya nchi na watanzania kwa ujumla,”ameandika Lema
Godi lesi.. Ulitarajia kuwemo katika hii panga pangua Kilaza Wewe...!!!
ReplyDeleteWenye ukiambia una macho mawili UTAJISHUKU...!!
Kiboko yako J.Muro na M.Gambo.
Hapa Kazi Tu.
Kama uko hai basi tutakufikiria huko 2029 .
Kwa sharti ikiwa utajirekebisha na kuwa Mzalendo mwenye kuwatumikia Watanzania
Si wa kuzunguka na kuuza filashi mjini.
Bei nasikia imeshuka na za mchina zimejaa Sokoni.. Nini strategy yako katika kuendeleza Biashara yako as a drastic recovery measure?
Kumbuka Awamu yetu hii ni inataka Uchape Kazi wakati wa Kazi ili Uishi. Vinginevyo utalala na Njaa. Lema