Hakuna kitu kinachoudhi na kuchanganya kama kuwa katika ndoa au mahusiano na mtu ambae hana uhakika ni nini haswa anataka. Unakuta kuna muda anaonesha kukupenda kweli, then baadae unakuta mtu huyohuyo anakufanya ujihisi hupendwi. Mtu anakuacha halafu baada ya kujitahidi kuendelea na maisha yako anarudi na kukuomba mrudiane.
Mtu anakwambia kabisa it's over, lakini baadae anakuita eti muyajenge. Mtu yuko na ndoa kabisa ila anajifanya yuko Single. Mtu kwa muda mfupi tu anabadilika kutoka "Nakupenda sana" kwenda "nakuchukia sana". Anakufanya unajisikia vizuri kidogo tu anakunadilikia..ni mbaya zaidi kama umezaa na mtu wa aina hiyo ambae haeleweki.
Huu upuuzi wa kutokueleweka kwenye mahusiano ni utoto. Mtu ambae amekua kiakili anahitaji uhakika. Mtu aliyekua kiakili anaeleza wazi kama mahusiano yapo au hayapo. Kuwa na uhakika na maamuzi yako kuliko kupotezeana muda.
Acha kumchezea michezo ya kitoto mwenzako. Chagua moja kama upo kwenye uhusiano nae au laa. Usiwe mguu mmoja ndani mguu mmoja nje. Mapenzi sio moody. Mapenzi ni kitu ambacho kipo constant. Mapenzi yanatabirika na yanayotegemeana. Mapenzi ni facts sio theory. Mpe mtu clarity kuhusu mahusiano yenu.
Ndoa imara na Mahusiano imara hayajengwi kwa misingi ya mapenzi yasiyo na uhakika. Mtu uliyenae anaweza kabisa kukubaliana na matokeo. Kama haumtaki tena mweleze wazi ili afahamu amesimama wapi. Ni bora kukataliwa sasa hivi ukaendelea na maisha yako huku ukijitahidi kutibu moyo, kuliko kuendelea kusalitiwa na mtu ambae hafahamu ni nini anachokitaka.
From Tweve Hezron