Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa uchumi wa nchi unazidi kudidimia na thamani ya shilingi inazidi kushuka huku mfumuko wa bei ukizidi kupaa.
Zitto Kabwe anasema kupitia Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ambayo jana ametoa taarifa yake juu ya hali ya uchumi nchini ni kwamba hali si nzuri kwani uchumi umeonyesha kusinyaa na kudidimia huku wananchi wa hali ya chini wakiwa wahanga wakubwa zaidi.
"Taarifa hiyo inaonyesha namna hali ya uchumi wetu inavyozidi kuwa mbaya zaidi kwa wananchi wa hali ya chini , kwa mfumuko wa bei umepanda mno tangu kuanza kwa utekelezaji wa bajeti ya 2017/18, ongezeko ambalo limechangiwa zaidi na kupanda kwa bei ya bidhaa za chakula (bidhaa ambazo wananchi wengi zaidi wanazitumia)" alisema Zitto Kabawe
Aidha Zitto Kabwe amedai kushuka kwa thamani ya sarafu ya Tanzania kumezidi kuongeza maumivu kwa wananchi na ili kusaidia kupunguza ukali na gharama za maisha mishahara ilipaswa kupanda kwa asilimia 8 zaidi.
"Thamani ya sarafu ya Tanzania imeshuka, uwezo wa Tsh. 100 kununua bidhaa umeshuka hadi Tsh. 92.18. Maana yake ni kuwa mwaka 2016 shilingi 100,000 ilikupa bidhaa za shilingi 100,000. Mwaka huu 2017 shilingi 100,000 inakupa bidhaa za shilingi 92,000. Kwa hiyo ili upate bidhaa za shilingi laki moja inakubidi uongeze shilingi elfu 8 zaidi. Kiuchumi, ili kulinda hali za wananchi, mishahara ilipaswa kupanda kwa asilimia 8 ili kuwapunguzia maumivu ya gharama za maisha. Lakini hali hiyo inatokea katika wakati ambao mishahara haijapanda, na Rais wa nchi yetu kasema Serikali anayoingoza haitapandisha kabisa mishahara. Hali ni mbaya mno mtaani, mijini uzalishaji wa bidhaa za viwanda umeshuka kwa zaidi ya nusu, kutoka trilioni 1.5 mpaka bilioni 700 tu" alisisitiza Zitto Kabwe
Mbali na hilo Zitto Kabwe ametoa ushauri wa nini serikali inapaswa kufanya ili kukabiliana na hali hiyo na kupunguza ukali wa maisha kwa wananchi, Zitto amedai Serikali inapaswa itazame namna inatekeleza mipango yake ya Maendeleo, Serikali isikilize na kufanyia kazi mawazo ya sekta binafsi katika kuweka sawa mazingira ya uwekezaji bila kupoka haki ya nchi kufaidi na rasilimali zake na pia ameitaka serikali ifanyie kazi haswa uchumi wa vijijini kwa kurekebisha mapungufu yote yanayoshusha uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.
Huyu Zito kabwe mcenge cumamaake. Yeye kila kukicha habari nzuri kwake zinazompelekea kujianika kwenye mitandao ni zile habari mbaya kwa nchi yetu unaona kabisa kwamba Zito kabwe hulala akiomba pengine hata kwenda kutambika ili taifa lifikwe na majanga apate cha kusema. Ukiniamabia Zito kabwe ni Mzalendo wa nchi yetu basi hapana shaka utakuwa una matatizo ya akili kama alivyo yeye wenyewe binafsi . Ukiangalia katika nchi zilizoendelea ambazo sisi tunaishi huku utakuta mwakilishi wa mkoa au jimbo fulani wala humsikii kupiga kelele za hovyo kuhusu hali ya nchi hasa katika masuala ya uchumi kwa sababu kabla hajapiga kelele kuhusu hali ya uchumi ya nchi hupigania jimboni kwake kwanza kuhakikisha hali ya uchumi ipo sawa. Na ndio maana hata ulipotokea mdororo wa uchumi duniani ndani ya nchi moja lakini kuna majimbo yaliendelea kuwa na uchumi imara mafano Texas kwa Marekani waliendelea kuwa na uchumi imara licha ya sehemu kadhaa za Marekani kuathirika. Na kufanya vizuri kwa Texas kiuchumi wakati huo wakati huo wa mdororo wa uchumi duniani haikuwa kwa bahati mbaya bali ni kutokana na viongozi na wadau wa mkoa huo wa Marekani au State kujikita zaidi kuhakikisha jimbo linakuwa na uchumi imara hahihalisi hali ya uchumi wa nchi kwa ujumla ipo vipi. Zito kabwe angekuwa anapigania hali ya uchumi wa kigoma na kutupasha maendeleo yake siku hadi siku. Zito nchi yake Tanzania lakini nchi yake halisi anayopaswa kuililia ni kigoma. Kigoma ikifanya vizuri hapana shaka Tanzania nayo itafanya vizuri. Zito kabwe nadhani unanielewa licha ya kutumia lugha ghasi hapo mwanzoni, matusi ni utamaduni wetu kuonesha kuchukizwa na kitu fulani katika levo ya juu kwa sababu unakera na unapoteza mwelekeo pengine kukuepusha yasikufike kama yaliyomfika rafiki yako Lisu believe me people have capable to do it again to someone else read sign of the time. Na usiwe mwanasiasa mpumbavu kwani unafahamu kabisa usemi usemao kama wewe ni Mzalendo wa kweli wa nchi yako basi don't cry like a baby and waiting for someone to do something for you except wake-up and not asking what country can do for you before asking yourself what did you do for the country. Zito kabwe Kukaa kusibiri kuilaumu serikali wakati huna mikakati yeyote ya maana kuisadia angalau mkoa wako wa kigoma kujikomboa kiuchumi na umasikini uliokithiri ni umasikini wa akili uliopitiza mipaka na ni wa kulaniwa kwa nguvu zote.
ReplyDeleteOfisi ya Taifa ya Takwimu.... ilimkaribisha lini huyu Kilaza.
ReplyDeleteOfisi ya Taifa ya Takwimu.... Haikuona Wachumi waliobobea katika fani hii mpaka wamualike Huyu Kilaza?
Ofisi ya Taifa ya Takwimu.... Wamefikia hadi ya Kuomba Mapendekezo na Ushauri wa Zitto?
Itabidi Ofisi hii na Wizara yake Husika Waihakiki hii Habari.
Zitto si mtu wa Kutueleza haya... Sisi tujuavyo ni kinyume na Haya.
Huyu Kilaza Baada ya kuondoka katika anga za Ukingo wa Siasa .. amehamia huko chini Feza Boki. Basi mwacheni huko huko tukitaka tutamfata na kuangalia afya ya ke ya Kiakili. Msituharibie blogi yetu ya udaku.... Zitto na upuuzi wake HATUUTAKI HAPA KWENYE BLOGU HII.
Huyu dogo anaeleweka na Amechanganyikiwa kuikweli. Na alisha karibishwa MIREMBE faili yake inamgoja kuanza kushughulikiwa Kimatibabu.
Tanzania yetu ni Salama na Hatuhitaji Mtafaruku wa kina Zitto na walio kama Wazitto Kubebwa.
Hapa Kazi Tu na Uchumi wetu unaimarika siku baada ya Siku.