Haya HapaMajina ya Mawazili Wanne Waliotemwa Uwazili

Haya HapaMajina ya  Mawazili Wanne Waliotemwa Uwazili
Rais John Magufuli amefanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kwa kuwatema mawaziri wanne waliokuwepo kwenye baraza la awali.

Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.

Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri Maji na Umwagiliaji,  Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi,  Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.

Panga hilo limempitia pia aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri tangu aingie madarakani.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera JPJM
    Hongera Mh Jassim Majaliwa.
    Hongrea Baraza La Zamani kwa kazi nzuri mloyofanyaHongera Baraza Jipya imani tunayo kwenu.
    Hongrra Watanzania nwebda Next Level.
    Dhamira inajulikana ni ufanisi na achèvement.
    Kila tunavyo endelea tunatini na ikihitajika na kubidi Magu hangoji tutafanya kwa Masilahi mapana ya Taifa letu na watu Wake.
    HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad