Hivi Ndivyo Halima Mdee Alivyomtahadharisha Nyarandu 'Naamini Utakuwa Imara Kukabiliana na Changamoto Tunazokumbana Nazo'

Hivi Ndivyo Halima Mdee Alivyomtahadharisha Nyarandu 'Naamini Utakuwa Imara Kukabiliana na Changamoto Tunazokumbana Nazo'
Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam Halima Mdee amemkaribisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini ndani ya chama chao huku akimtahadharisha  kuhusu changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa chama hicho.

 Halima Mdee ametumia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha Nyalandu ambaye leo ametangaza kujiuzulu nafasi zake za uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na nafasi yake ya ubunge aliokuwa nao.
"Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu".
Mapema leo Mh. Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM litangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwa na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ARUDISHE KWANZA TWIGA WETU ALIWAPANDISHA NDEGE KIPINDI ALIPOKUWA WAZIRI WA MALIASILI PIA HATA AKIKIMBIA AKITEGEMEA HUKO NDIO KIMBILIO AJUE KWAMBA ATASHITAKIWA TU KWANINI ALIPANDISHA TWIGA NDEGE? ANAONA PANGA LINAHAMIA KWENYE MALIASILI BAADA YA KUTOKA KWENYE MADINI ANAAMUA KUHAMA TUMEMSITUKIA ASIFIKILI HATUMUELEWI TUNAMUELEWA SANA HUYO TUNATAKA TWIGA WETU ALIWAPANDISHA NDEGE KWANZA

    ReplyDelete
  2. Mbona hakudaiwa hao Twiga akiwa hajahama? au akiwa ndani ya system sio mwizi ila akihama ndipo alama za wizi huonekana? je twiga wakati wanasafirishwa ndani ya ndege ya Katari mwaka 2010, Nyalandu alikuwa waziri? Wakati wa operation tokomeza ujangiri iliyoaacha watu na majonzi Nyalandu alikuwa waziri?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad