Nigeria yakosoa Sanamu ya Rais Jacob Zuma

Serikali ya jimbo moja nchini Nigeria imempa heshima rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, kwa kumjengea sanamu kubwa ya shaba na kuipa barabara moja jina lake.

Wakati akifanya ziara katika jimbo lililopo kusini mashariki la Imo siku ya Jumamosi na Jumapili, Bw. Zuma alipewa cheo cha kiongozi wa kitamaduni ambacho ndicho cha juu zaidi kinachotolewa eneo hilo.

Muungano wa mashirika ya kupambana na ufisadi (CSNC) ambao ni wa zaidi ya mashirika 150 ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria, umemlaani gavana wa jimbo Rochas Okorocha, kwa kumtambua Zuma kama mtu shujaa mbele ya kundi la vijana wa Afrika, wakati anakabiliwa na shutuma nyingi za ufisadi nchini mwake.

"Ni kama Gavana Okorocha hafahamu kuwa watu wa Afrika Kusini kwa sasa, wanamtaka rais wao ajuzulu kwa kuleta aibu kwenye nchi ya Nelson Mandela?" uliandika katika taarifa.

Pia taarifa hizo zimekosolewa vikali katika mtandao wa twitter.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad