Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro ameagiza wafanyabiashara na watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi nchini kuchukuliwa hatua kali kwani wanarudisha nyuma na kuchelewesha maendeleo ya nchi.
IGP Sirro amesema hayo jana alipofanya ziara mkoani Mbeya na kuwaagiza askari wa vikosi mbalimbali vya polisi kuhakikisha wanawakamata na kuwachukulia hatua za kisheria watu wote ambao wanakwepa kulipa kodi.
"Kuna watu wanafikiri ni sifa kufanya magendo wote tunajua umuhimu wa kulipa kodi kwa hiyo tumepanga mpango mkakati wa kuwashughulikia vizuri sana wale ambao wanakwepa kulipa kodi, wananchi wetu wanapaswa kubadilisha mtazamo wao waone wanawajibika kwenye kulipa kodi sababu kodi ndiyo inafanya maendeleo ya nchi yetu, kodi ndiyo inaleta madawa, kodi inaleta barabara na kodi ndiyo kila kitu. Na wale ambao wanakwepa kulipa kodi nimetoa maelekezo kuwashughulikia kila mahali na kila siku wanasikia Amiri Jeshi Mkuu anazungumzia habari hii sasa wewe unayekwepa kulipa kodi ni nani" alisisitiza Sirro
Aisha IGP Sirro aliwataka wafanyabiashara pamoja na wananchi kulipa kodi ili nchi iweze kupata maendeleo na kusonga mbele zaidi.
Kamanda Sirro, Hongera kwa Hili.
ReplyDeleteSisi wote ni Lazima Tumsaidie Mh Raisi JPM kuona Dhamira endelevu ya Kututumikia Inatekelezwa na Kila Mmoja wetu katika Nafasi yake ya Utumishi na Majukumu.
Kodi ni Muhimu na Athari zake za Ulibikizaji na Ukwepaji. Hupeleka Taifa kushindwa Kukidhi na Kutatua Kero na Adha za Wananchi tukiwemo mimi na wewe.
Na Asiyelipa ni lazima Tumshughulikie na Mlimbikizaji Sugu ni Lazima tumpige Tanchi ili apate fundisho na somo kwa wengine.
Siyo vyema kukwepa Kodi na Wala hatutomvumilia Mkwepa Kodi.
Tanzania ni ya Watanzania wenye Utashi wa kuona TANZANIA MPYA INAKUJA....Hongera Kamda Sirro,
Hongera Mwigulu na Hongera Mh.K.Majaliwa katika nafasi mlizopewa na Baba JPJM.
TUTAFIKA KWA PAMOJA NA WAXHELEWESHAJI HATUWATAKIIIIIII .....!!!! KWAMWE.
Mkulu Alibaho!!! Milimo Ilibaho.... HAPA KAZI TU.