IGP Sirro Aomba Msaada Kutoka kwa Viongozi wa Dini

IGP Sirro Aomba Msaada Kutoka kwa Viongozi wa Dini
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP simon siro amewaomba viongozi wa dini na wanasiasa mkoani iringa kushirikiana katika kutokomeza vitendo vya ulawiti na ubakaji ambavyo vinazidi kushamiri mkoani humo.

IGP  Siro Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani iringa.
IGP Siro amesema kuwa ili vitendo hivyo vitokomezwe ni lazima elimu izidi kutolewa kwa jamii hususani masuala ya imani za kishirikina ambayo yametajwa kuwa chanzo kikubwa cha kuchangia matukio hayo .
"Hili ni tatizo kwa watanzania inabidi elimu iendelee kutolewa sana. Tuna kazi kubwa ya kutoa elimu kwa hao ndugu zetu. Hayo mambo yalishapitwa na wakati, huwezi kupata utajiri kwa kumbaka mtoto wa umri wa  miezi miwili hadi mitatau. Tunaomba sana viongozi wa dini na siasa watusaidie katika hili. Sisi kama chombo cha dola tuna wajibika sana katika hili kwani elimu ni kitu cha kwanza kabla ya kutumia sheria, ili hata akifanya baadae akiwa na elimu unajua kabisa huyu anafanya makusudi," amesema Kamanda Sirro.
Aidha IGP Sirro  amezungumzia suala la watu ambao wamemshambulia mbunge wa Singida Mashariki  hivi karibuni Tundu Lissu na kusema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo.
Sambamba na hayo, amewasihi askari kufanya kazi kwakuzingatia misingi ya sheria bila kumuonea mtu yoyote kwakuwa hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad