IGP Sirro: Mjadala wa Tundu Lissu kupigwa risasi ufungwe mara moja

Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro ametaka mjadala kuhusu kupigwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, ufungwe mara moja.

Agizo hilo amelitoa leo akiwa ziarani jijini Mbeya wakati akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo amewaonya wanasiasa kuacha kuuendeleza na waliachie jeshi lifanye kazi yake.

Kuhusu madai yaliyotolewa hivi karibuni na familia ya mbunge huyo kuwa jeshi hilo halina dhamira ya dhati ya kufanya uchunguzi, IGP Sirro amesema hana cha kuwajibu kwa kuwa hataki malumbano na familia hiyo.


Chanzo: Azam Tv
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad