Inakuwaje Kuna Pato la Taifa Linakuwa Wakati Wananchi Wanalalamika Hali Mbaya Vyuma Vimekaza- Zitto Kabwe

Inakuwaje Kuna Pato la Taifa Linakuwa Wakati Wananchi Wanalalamika Hali Mbaya Vyuma Vimekaza- Zitto Kabwe
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Mh.Zitto Kabwe amesema kuwa wanasikia pato la taifa linakuwa na ni miongoni kati ya nchi 20 ambalo pato la taifa lina kuwa kwa kasi wakati anasikia malalamiko ya wananchi wanasema hali mbaya na vyuma vimekaza.

Zitto ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu Takwimu za pato la Taifa amesema kuwa ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuaje tuna pato la taifa linalokuwa yani miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana lakini wakati huo huo wananchi wanalia.

“Tunasikia pato la taifa linakuwa na ni miongoni kati ya nchi 20 ambalo pato la taifa linakuwa kwa kasi kuliko nchi zingine lakini wakati huo huo mnasikia malalamiko ya wananchi wanasema hali mbaya, vyuma vimekaza sasa ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuaje tuna pato la taifa linalokuwa yani miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi sana lakini wakati huo huo wananchi wanalia kwamba vyuma vimekaza kwamba hali ni mbaya,” amesema Zitto.

“Kwanini sasa miaka ya nyuma tulikuwa hatutazami na kwakweli hata tulipotazama safari hii tumekuta miaka ya nyuma hakuna shida yani mpaka mwezi Machi 2017 takwimu zilizokuwa zinatolewa na serikali na takwimu ambazo unazikokotoa kutokana na hali ya uchumi na kanuni za uchumi hazina utofauti zilikuwa sawa kabisa lakini takwimu za mwezi AprilI,Mei,June zimeonyesha tofauti kubwa sana na ndicho kilicho tuletea mashaka.”

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huu ni upumbavu mwengine kutoka kwa Zito Kabwe kama ni kweli hiyo mada ya hapo juu ni yake halisi? Zito labda amewahi kutembelea nchi mbali mbali duniani hasa zile zilizoendelea nakuona hali halisi za maisha ya watu wao wote kama hajaona mimi nitampa mfano mmoja katika mingi. Zito aliwahi kuumwa siku za nyuma nakama sikosei alikwenda au kupelekwa India kwa matibabu. India ni nchi zinazokuwa kwa kasi ya ajabu kiuchumi maendeleo na unaweza kusema au kuita ni nchi iliyoendelea tayari lakini nenda kasikilize maoni kuhusu maisha ya wahindi mmoja mmoja wengi wao unaweza ukashangaa kabisa kutokana na wanavyoteseka na hali ngumu ya maisha. Kufanya vizuri kwa pato la taifa sio kigezo cha haraka na kwa kila mwananchi awe na hali nzuri ya maisha. Kwa kawaida binaadamu mwenye kujitambua anapofikwa dawa sio kalalamika bali ni kukabiliana nao kikamilifu na kutafuta ufumbuzi. Dunia inapoelekea hivi sasa kama wataalamu wanavyosema inaelekea kubaya kiasi cha kutishsia uwezokanao wa kizazi cha sasa kutoweka dunianai baada ya muda mfupi na hii yote ni kwa sababu upoteaji wa kutisha wa maadili kwa binaadamu wa sasa kwa kisingizio cha demokrasia. Usenge na usagaji ni halali karibu nchi nyingi duniani hivi. Na mwiitikio wake kwa vijana na kwa wazee ni wa hali ya juu kushiriki kwenye tendo hilo. Vijana wanahamasishwa kutotii mamlaka za serikali zao ni kosa ambalo limekemewa hata kwenye vitabu vya dini kwani hata wanyama porini wana kiongozi wao na wanamtii. Umon'gonyekaji wa maadili inasemekana ni tishio kwa uwezo wa kuwepo binaadamu hapa duniani kuliko hata silaha za Nyuklia. Mungu hakumuumba binaadamu afanye kila atakalo bila kuchunga mipaka yake. Demokrasia sio sababu ya ukosefu wa heshima na adabu kama tunavyoshuhudia kutoka kwa baadhi ya watu wa upinzani nchini. Utashangaa kwanini nchi kama Marekani iwe na homless wengi pengine kuliko hata nchi nyingi masikini.Licha ya kuwa Marekani ina idadi kubwa ya watu lakini hii Marekani bana? Kuwa homless natafuta neno sahihi kwa kiswahili lakini hali ya mwisho wa uduni wa mwanadamu katika maisha. Mtu hana pa kulala, hajui atakula wapi, atajisaidia wapi mara nyingi huishia kujisadia kwenye makazi ya watu wengine nakadhalika nakadhalika vile vike inapaswa tuulize kwanini nchi kama Marekani ina watu wa aina hiyo na wengi wao ni wamarekani halisi wasiowahamiaji? Zito inabidi apanuke kiakili aache kuiliza masuala ya kipuuzi.

    ReplyDelete
  2. Huyu Dogo ana matatizo ya kiafya ya ubongo.
    Anajifanya kutafuta kiki toka nchini twita na ukachero wa kujua na kujiaminisja kuwa mapungufu ya serekali ya awamu ya tano yako mezani kwake.
    Umepotoka mwaya... usipotoshe umma.
    Sisi Wazalendo tina imani na KPKM na serikali yake teule.
    WACHA POROJO ZAKO DOGO.
    TAFUTA PLAY STATION UCHEZE GTA GAMES.ZINAKUFAA KAMA HUWEZI KURUDI KIGOMA KUWALETEA MARNDELEO WALIOKUPA KURA HAWA HATA MASHINE ZA KUTENGENEZA BARAKU KWA AJILI YA SAMAKI.
    MWAYA MBONA HUELEWEKI NA HUJIELEWI.
    KOMENTI KOMENTI USIYOKUWA NA UJUZI AU WELEDI NAYO...PWAAA PWAAAA

    ReplyDelete
  3. ahaa Jito...!!! upo?? anga zipi
    unaliamsha Dude.!!!
    Kimenuka....!!!
    Ndiyo zako...au vp.
    Unazipenda...!!!
    mie naiza playstatiom yangu sekand hendi.. Bei poa.
    na bando ya cd bure ikiwemo
    Grand theft Auto.
    utapoteza wakati kwa Burudani Murua.
    ulikwenda ofisini...leo. mlango Imesindikwa...Funguo mnnazo.
    We Dogo umekuwa mchumi siku hizi.!!!??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad