Israel Yadai Kuwaona Wadukuzi wa Urusi Wakiidukua Marekani

Israel Yadai Kuwaona Wadukuzi wa Urusi Wakiidukua Marekani
Majasusi wa Israel waliwaona wadukuzi wa Urusi wakidukuwa programu ya kuzuia virusi mitandaoni Kaspersky kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.
Warusi hao walidaiwa kujaribu kuchukua data kuhusu mipango ya ujasusi ya Marekani kulingana na gazeti la New York Times na Washington Post.
Majasusi wa Israel walibaini hayo baada ya kuidukua programu hiyo.
Mfumo huo wa usalama kwa jina Kaspersky umesema kuwa haikushirikishwa wala haukugundua kuhusu hali hiyo na imekana kushirikiana na serikali yoyote.
Mwezi uliopita, serikali ya Marekani iliamua kusitisha udukuzi huo kupitia programu hiyo ya Urusi katika kompyuta zake.
Waisraeli hao wanadai kuijulisha Marekani , hatua iliosababisha kupigwa marufuku kwa programu ya Kaspersky.
Gazeti la The New York Times lilisema kuwa hali hiyo ilielezewa na watu kadhaa ambao walielezwa kuhusu swala hilo.
Nakala kadhaa zimedaiwa kuibwa kutoka kwa afisa mmoja wa ujasusi wa Marekani ambaye alikuwa ameweka programu ya kaspersky ili kulinda virusi katika kompyuta yake.
Hakuna matamshi yoyote yaliotolewa na Shirika hilo la ujasusi la Marekani NSA, ikulu ya Marekani na ubalozi wa Israel.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad