Jeshi la Polisi nchini kitengo cha mitandaoni ya kijamii kimewataka viongozi mbalimbali wa makundi ya WhatsApp nchini kutoa taarifa katika jeshi hilo pindi uhalifu unapofanyika kwenye makundi hayo na kusema wao watashughulika na wahalifu hao.
Naibu Mkuu wa Kitengo cha Polisi Mitandao ya kijamii, Joshua Mwangasa kwenye semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Kamati ya Amani ya viongozi wa dini Jijini Dar es Salaam.
"Kuna makundi mengi ya WhatsApp lakini yalikuwa makundi kwa ajili ya kupeana taarifa ambazo ni za msingi kwa mfano kama sisi tunavikundi vya dini, tuna taasisi ilikuwa ni kufahamishana kwamba jamani kuna ujumbe huu lakini sasa watu yale makundi wanayatumia kama sehemu ya kufanya uhalifu kule, sehemu ya kutupa mapicha ambayo hayastahili sasa si kila mmoja ambaye anapendezewa na hicho kitendo, kwa hiyo lazima tuchukue hatua ya kuweza kuripoti polisi kwamba kuna tukio hili na lile na namba fulani ndiyo inatuma sisi tuko tayari usiku na mchana kupambana kuona kunamfikia huyo mtuhumiwa" Alisema Joshua Mwangasa
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA amewataka viongozi wa dini nchini kutumia nyumba za ibada na nafasi zao katika jamii kulinda maadili katika jamii na kuhakikisha kuwa matumizi bora ya mitandao ya jamii yanafikiwa.