Jeshi la Polisi Latoa Tamko Mauaji Askari Ukonga

Jeshi la Polisi Latoa Tamko Mauaji Askari Ukonga
Jeshi la Polisi Kanda Maalum jiini Dar es salaam, limesema linalaani vikali vitendo vya mauaji ya askari wake wa kikosi cha kutuliza ghasia Ukonga, yaliyotokea sikuchache zilizopita.

Taarifa hiyo imetolewa na  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ambapo pia amelaani vikali kitendo cha askari wa jeshi la polisi kuvamia wananchi na kuwapiga, akisema si jambo sahihi kwa askari kufanya hivyo na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.
"Tunalaani vikali mauaji ya askari wa polisi wa FFU kikosi cha Ukonga, lakini sambamba na hilo jeshi la polisi linalaani vitendo vya kihuni vya wananchi kushambuliwa, kuna watu wahuni ambao wanasambaa usiku wanakamata wananchi, kuwapiga na kuwadhalilisha kina mama na wengine kujeruhiwa, hakuna askari wa jeshi la polisi aliyefundishwa anayeweza kuyafanya hayo yanayoelezwa kufanyika, na kama atabainika ni kweli ni askari, watakamatwa, watahojiwa na tutawashughulikia kijeshi na kama wahalifu wengine watafikishwa mahakamani", amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa ameendelea kwa kusema kwamba jeshi hilo linaendelea na upelezi dhidi ya watu waliomuwa askari wake Charles Yanga wa kikosi cha Ukonga, na watakapobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad