Jeshi la Polisi Lavamia Mkutano waSeik Ponda Waanishi wa Habari Wakamatwa

Jeshi la Polisi Lavamia Mkutano waSeik Ponda Waanishi wa Habari Wakamatwa
Jeshi la Polisi nchini limevamia mkutano wa Sheikh Issa Ponda ambao ulikuwa unatakiwa kufanyika katika hoteli ya Iris, Kariakoo jijini Dar es Salaam ambapo alikuwa amepanga kuzungumzia sakata la Tundu Lissu kupigwa risasi.

Mwenyekiti wa kamati ya uongozi ya CUF, Julius Mtatiro amethibitisha polisi kuzuia mkutano huo na kusema kuwa baadhi ya waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye ukumbi huo wamekamatwa na polisi.
"Polisi wamevamia mkutano wa Sheikh Issa Ponda katika hoteli ya Iris, Kariakoo. Taarifa za awali zinasema baadhi ya waandishi wamekamatwa. Sheikh Ponda alikuwa azungumze na vyombo vya habari kuhusu suala la Kupigwa risasi kwa Tundulissu asubuhi hii, mara baada ya kurejea kutoka Nairobi ambako alizungumza na Lissu" alisema Mtatiro.

Sheikh Issa Ponda alikwenda kumtembelea, Tundu Lissu hospitali Nairobi nchini Kenya ambako anapatiwa matibabu kufuatia kushambuliwa kwa risasi Septemba 7, 2017 mjini Dodoma na baadaye kupelekwa Kenya kwa matibabu zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad