Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kuwafukuza kazi Wakurugenzi wa halmashauri wanne kwa ulevi wa pombe pindi wawapo makazini.
Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema hayo alipokuwa kwenye Mkutano wa 33 wa Jumuiya Ya Tawala za Mitaa (ALAT) ambao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam na kusema amepata taarifa kuwa wapo Wakurugenzi kadhaa ambaio ni walevi na kudai wasipobadilika ndani ya muda mfupi atawafukuza kazi.
"Nimepata taarifa ya Wakurugenzi kama wawili watatu hivi ni walevi sana, nawaambia hao wataondoka kama upo hapa Mkurugenzi halafu ni mlevi ukajirekebishe haraka sana, kabla sijaja huko ili angalau uonekane umebadilika" alisema Rais Magufuli.
Mbali na hilo Rais Magufuli aliwataka viongozi hao kwenda kumaliza migogoro mbalimbali ndani ya halmashauri zao na mivutano isiyokuwa na msingi na kusema kuwa vyama vya siasa si adui bali adui wa kwanza wa serikali yake ni watu wanaokuja kuiba maliasili za Tanzania.
"Haipendezi kuwa na makundi muyamalize makundu hayo kwenye manispaa, tunajenga nyumba moja adui yetu siyo vyama tunachelewa sana, adui yetu ni wale wanaotuibia nasema mkamalize hayo makundi huko, najua tofauti lazima zitakuwepo lakini kwenye masuala ya kazi lazima tushikamane kwa maslahi ya Watanzania, mkawaimize Watanzania kufanya mambo ya maendeleo" alisisitiza Rais Magufuli