Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, amemteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, baada ya aliyepo sasa, Gavana Benno Ndulu kumaliza muda wake, miezi michache baadaye.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akiunuku vyeti kwa kamati zilizofanya uchunguzi wa kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia, ikulu jijini Dar es Salaam.
kabla ya uteuzi huo, Luoga ambaye kitaaluma ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na uteuzi wake utaanza baada ya Benno Ndulu kumaliza muda wake.
JPM Amteua Profesa Florens Luoga Kuwa Gavana wa BOT
0
October 23, 2017
Tags