Kampuni ya Barrick Yakubali Masharti Yote ya Sheria Mpya ya Madini

Kampuni ya Barrick Yakubali Masharti Yote ya Sheria Mpya ya Madini
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesema kuwa kampuni ya Barrick imekubali masharti yote ya sheria mpya madini mazungumzo yao.

Profesa Kabudi amesema hayo leo Alhamisi wakati akitoa taarifa kwa Rais John Magufuli kuhusu majadiliano kati ya Serikali na kampuni ya Barrick.

“Pia wamekubali Serikali kuwa na asilimia 16 kwenye migodi yote ya Barrick na kwamba kwenye mgawanyo itakuwa ni asilimia 50 kwa 50.

Amesema mbali na hilo pia mapato yote ya kampuni hiyo yatawekwa kwenye akaunti zilizopo hapa nchini na kwamba makao makuu yao yajengwe Mwanza.

Amesema mbali na hilo pia kampuni hiyo imekubali kuwa kila kampuni inayoendesha migodi kuachana na wafanyakazi wa mikataba bali waajiriwe wazawa na wasiwe wanakaa kambini.

“Hii ni kuachana na mtindo wa sasa wa kuwaweka watu wazima kwenye makambi,”amesema Profesa kabudi.

Awali Mwenyekiti Mtendaji wa Barrick, John Thonton amesema makubaliano hayo yataenda kuidhinishwa na Bodi nchini Uingereza ambayo ina hisa asilimia 64.

Amesema wamekubaliana pande hizo mbili watakuwa wanagawana faida asilimia 50 kwa 50 kama alivyosema Profesa Kabudi.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hongera kea Bateick na Watanzania kea ujumla.
    Cha muhimu baada ya hapa Ni malimbikizo na wizi je wanTulipaje. Hata kea awamu watanzania Ni waelewa. Matriliono yetu hat to yaachia.
    Na mikataba nao SI ya kudumu kwishakila. Miaka 4 tunasaini nao upya na tunafloat operational and production tenders huko duniani. We Hate Economical Hitman's. Kama wake akasia ambao tutapiga marufuku hili jina hapa nchini na ballick wapatowe leseni halali baada ya kiwasilisha maombi halali nchini ambayo yanaqwza kufikuriwa na kukubaliawa au kukataliwa mpaka waturidhishe na Nia husika
    Kabudi mlingu akutaze mwana mlimo Wamalika...salamaaje wadodo kukaya.
    HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. KAMA-NAWAONA-WALE-WAPINGA-KILA-KITU-----WATANUNAJE?? hahahaha

    HONGERA-MKUU-JPM.........HAPA-KAZI-TU, MAJUNGU-NA-LONGO-LONGO-TUPA-KULE

    ReplyDelete
  3. Mungu akubariki JPJM.
    Isingekuwa wewe madaraka I.. Kweli tungetaona haya.
    Ngosha... Mwangaluka wiza...!!!
    Mungu akuweke uendelee kututumikia kea Nia na Roho hii hii...!!!
    Na sasa Mama Kairuki PIA mtamboni...kwa ubunifu wake na utendaji wake ..mungu amsaudie na sisi PIA tuwe kitu kimoja katika kuileta Tanzania yetu MPYA.
    PROF KABUDI NATIMU ZOTE HUSIKA..KAZI TULIYOWAPA TUMEONA MATOKEA NA BADOOOO MNAENDELEA NAYO MPAKA LIYAMBA.
    HONGERA SANA.
    JPM NIA YAKO NA MSIMAMO WAKO NDIYO ...HAYA MATUNDA YANAANZA ENDELEZA MIUNDI MBINU KUTURAHISISHIA MAENDELEO YA VIZAZI VIJAVYO.
    TUNAKUOMBEA NA TUNAENDELEA KUKUOMBEA USIKU NA MCHANA KATIKA SALA ZETU INSHA'ALLAH.

    ReplyDelete
  4. Ni faraja na fahari kwa Taifa letu, wapo watakaoendelea kubeza na kupinga lakini hawatokuwa na jipya, tumeshawazoea, Hongera sana JPM "avec toi toujours', bon travail"

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad