Majina ya watu waliokuwemo kwenye Ndege moja aina ya Helikopta ambayo ilihusika katika ajali Jumamosi asubuhi katika Ziwa Nakuru nchini Kenya, yametolewa. Kwa mjibu wa kanmshena wa kaunti ya Nakuru, Joshua Nkanatha, ndege hiyo ya Helikopta ilikuwa njiani kuelekea maeneo ya Narok ambapo Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ahutubie mkutano wa kisiasa, siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Urais Oktoba 26, ajali hiyo ilipotokea.
Majina ya wahasiriwa ambao bado hawajapatikana ni Bwana Sam Gitau, John Mapozi, Anthony Kipyegon na mwanamke aliyetambuliwa tu kama Veronicah, pamoja na rubani wa ndege hiyo Bwana Apollo Malowa. Hadi sasa watano hao hawajulikani waliko.
Ndege hiyo pia ilikuwa imepangiwa kuwabeba waandishi wa vyombo kadhaa vya habari nchini Kenya.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na wakuu nchini Kenya, zinasema kuwa abiria wa ndege hiyo pamoja na rubani walikuwa walevi- Kwani walikesha usiku kucha wakinywa vileo katika maeneo kadhaa ya burudani mjini Nakuru.
Ndege hiyo ya helikopta aina ya 5Y-NMJ ilianguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi baada ya kuondoka katika hoteli moja mjini humo.
Afisa mkuu wa Polisi mjini Nakuru Joshua Omukata amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akikanusha taarifa kuwa ndege hiyo inamilikiwa na Rais Uhuru Kenyatta. Ndege hiyo inadaiwa kumilikiwa na kampuni ya Flex Air Charters, na kusimamiwa na Kapteni Bootsy Mutiso.
Aidha, amesema kuwa shughuli za kutafuta mabaki ya ndege hiyo na miili ya wahasiriwa zinaendelea.
Ripoti zinasema kuwa kulikuwa na watu watano katika ndege hiyo.
Seneta wa Nakuru Susan Kihika amesema kuwa watatu kati ya wale waliokuwa wameabiri ndege hiyo, walikuwa wanachama wa kitengo chake cha mawasiliano.
Kwa mjibu wa kanishena wa kaunti ya Nakuru, Joshua Nkanatha, ndege hiyo ya Helikopta ilikuwa njiani kuelekea maeneo ya Narok ambapo Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ahutubie mkutano wa kisiasa, siku chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu wa Urais Oktoba 26, ajali hiyo ilipotokea.
Ndege hiyo iliondoka katika hoteli ya Jarika County Lodge na duru zinasema kuwa ilikuwa ikipaa chini chini kabla ya kuanguka.
Ndege hiyo ilitarajiwa kusafrisha waandishi wa habari katika mkutano wa kampeni za Rais Uhuru Kenyatta.
Waokoaji walilazimika kusubiri boti kusafirishwa kutoka Ziwa Naivasha.
Mkurugenzi wa Idara ya kitaifa ya kukabiliana na majanga Pius Masai amesema kuwa ndege ya polisi imetumwa katika eneo hilo kusaidia katika uokoaji.