KENYA: Raila Odinga(NASA) Ajitoa Kugombea Urais wa Kenya Uliokuwa Ufanyike 26 Oktoba 2017

Raila Odinga ajiondoa kugombea urais wa Kenya, kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 26, 2017

Miongoni mwa sababu kubwa za kujitoa ni;
Wamehisi kuwa IEBC haina nia ya kuhakikisha yale makosa yaliyosababishwa kufutiliwa mbali matokeo ya urais Augost 8 kuwa hayatajirudia tena.
Pia wameona wapianzani wa Jubilee wataka kufanyia Katiba mapinduzi na kurudisha udikteta, wanaona kuwa Jubilee wanataka tu kuwe na uchaguzi ila wao wanataka uchaguzi bora
Pia IEBC kutokufuata masharti waliyotoa ambayo yangeakikisha kuwepo kwa uchaguzi bora na wa haki


“Kwenye demokrasia ya Kikatiba, hatakiwi kulumbana kuhusu uchaguzi huru na wa haki. Tulitakiwa tushirikiane kwa kufanya kazi pamoja kuhakikisha tunashikilia maadili haya ambayo sio tu maadili ya taifa letu bali pia ni msingi wa mfumo wa uchaguzi wa kuaminika”

"Tumeshinda vita ya demokrasia ya vyama vingi na ya Katiba mpya. Tutashinda vita ya uchaguzi huru na wa haki"

Wakati huo huo, Raila Odinga amewataka wafuasi wake nchi nzima kuandamana kesho kupinga kitendo cha Tume ya Uchaguzi kugoma kubadili uongozi wake.

Baada ya Tamko hilo, Mbuge Ndindi Nyoro amesema;
Kwanza mimi nafurahi sana vile amejiondoa kwa sababu ni kuonyesha wakenya ya kwamba vile tumekuwa tukisema kama watu wa Jubilee, NASA haijawahi kuwa ready kwa elections. Tulianza 8 august even before that walikuwa wanashinda kortini kulalamika huko.

Hii ni kwa sababu hawa-take any chance ya ku-face wakenya.

Maoni yangu ni kumuapisha rais wetu Uhuru, kwa sababu hatuwezi kuwa na mtu mmoja kwa sababu ya greedy yake ya kuongoza watu anazungusha nchi yetu kila siku

VIDEO:
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad