Kiama Chaja: Bomoabomoa ya Kufa Mtu Kuikumba nchi Nzima! Ni Kwa Waliojenga Bila Vibali

Serikali imewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka alama za X na kuvunja majengo yote yanayojengwa katika miji yao bila kibali na yale yanayojengwa katika viwanja vya watu wengine walio na hati miliki zao za ardhi kwa dhuruma.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameyasema hayo alipofanya ziara wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa alpoenda kutatua mgogoro wa ardhi ambapo ameagiza eneo ya lililokuwa shamba la mifugo la Malonje wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa lenye ukubwa wa ekari 12,750, lirejeshwe serikalini kwa vile utaratibu wa kuligawa umekiukwa kwa kiwango kikubwa, na masharti ya uendeshaji hayajazingatiwa kabisa.

Waziri Lukuvi amesema tatizo la ujenzi holela lianaanza pale ambapo Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji wanawaacha majengo yanaibuka katika miji yao bila kujua ujenzi huo una kibali au unajengwa katika kiwanja chenye hati na muhusika wa hati hiyo ndio anayejenga.

“Hatuwezi kuendelea na zoezi la kufanya urasimishaji wa makazi kila siku wakati chanzo cha tatizo hilo kinajulikana, kwa hiyo naagiza Wakurugenzi, Maafisa Ardhi, Maafisa Ujenzi na Maafisa Mipangomiji kuweka X katika majengo yote yanayojengwa bila vibali na ujenzi unaofanywa kwenye viwanja vya watu masikini kwa dhuruma” amesema Lukuvi.

Lukuvi amesema atapambana na viongozi hao pale ambapo atakuta majengo yamekithiri katika miji yao na hayana vibali vya ujenzi na baya zaidi majengo hayo yamejengwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kujenga au yamejengwa katika kiwanja cha mtu mwingine na viongozi hao wameshindwa kufuatilia kwa kuyavunja au kuyaweka alama ya X majengo hayo, kwa kuwa huu ni uzembe unaotokea nchi nzima.

 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen amemhakikishia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kuwa atayafanyia kazi mapendekezo yake kikamilifu na kwa haraka ili kuondoa migogoro na kero zinazoukabili mkoa wake katika masuala yote ya ardhi.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amesema Serikali imekusudia kuwanyang’anya mashamba watu wote waliokodishwa kwa kuyatumia kama dhamana kwa ajili ya kupata mikopo kutoka kwenye mabenki ndani na nje ya nchi lakini mikopo hiyo hawaitumii kuinufaisha nchi wala kuiendeleza ardhi waliyoitumia kama dhamana.

Waziri Lukuvi ameongeza kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya wawekezaji wengi wenye mashamba makubwa kutumia ardhi kama dhamana kwa ajili ya kupata mikopo kutoka kwenye mabenki ndani na nje ya nchi lakini mikopo hiyo wanaitumia kuwekeza nje ya nchi na kujenga majengo nchi za Ulaya, dubai na kwingine duniani.

Lukuvi amesema Haiwezekani mtu atumie ardhi yetu kujipatia fedha halafu fedha hizo azitumie kuendeleza nchi nyingine na kuiacha ardhi yetu kama pori jambo ambalo linaleta migogoro mikubwa katika jamii inayoyazunguka maeneo hayo.

“Kwa hiyo Wizara yangu imekusudia mwezi ujao kupeleka Bungeni marekebisho ya sheria namba 24 ya mwaka 1999 ili kuongeza vifungu ambavyo vitadhibiti mikopo inayopatikana kwa kutumia ardhi kama dhamana” amesema Waziri Lukuvi.

Marekebisho haya tunalenga kuwezesha fedha zinazopatikana kutokana na mikopo iliyotolewa itumike kuendeleza sehemu ya ardhi husika iliyotumika kama dhamana ya kuomba mkopo katika mabenki. Kwa kuwa Tathmini iliyopo inaonesha, baada ya wekezaji hao kupata mikopo kwa kutumia ardhi kama dhamana fedha hizo hawazitumii kuendeleza ardhi husika au katika uwekezaji wowote hapa nchini.

Lukuvi amesema, kuanzia mwezi Novemba tatizo hilo litakwisha kabisa kwa kuwa jukumu hili yatapewa mabenki na wakopeshaji wote ambao watafuatilia kwa karibu maombi ya mikopo kutokana na mpango mkakati uliowasilishwa katika Benki husika.

“Na kama Benki husika haitowafuatilia na kuamua kumuachia mtu huyo kwa kuwekeza fedha hizo anavyotaka bila kuendeleza ardhi husika, basi Serikali itamyang’anya mkopeshwaji huyo shamba hilo kwa kuwa atakua amekiuka sheria halafu Benki ambayo itamuachia mtu achukue fedha na asiendeleza shamba lile itakuwa imekula hasara yenyewe” amesema Waziri Lukuvi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad