WATAHINIWA wapatao 385,938 wameanza kutafanya mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne leo Jumatatu, Oktoba 30, 2017 kote nchini. Akizungumza jana Jumapili, Oktoba 29,2017 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde alisema kati ya watahiniwa hao, 323,513 (School candidates) ni wa shule na 62,425 ni wa kujitegemea (Private candidates).
Dk Msonde alisema mitihani hiyo itaanza leo Oktoba 30, 2017 na kumalizika Novemba 17, 2017 huku akieleza kuwa maandalizi ya mitihani yameshakamilika na mitihani imeshafika kwenye vituo.
Aidha Msonde alizitaka kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa mitihani hiyo unafuatwa huku akiwataka wanafunzi kuacha vitendo vya udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila kufanya hivyo.
“Mliyojifunza yanatosha fanyeni mitihani kwa kufuata utaratibu uliowekwa, baraza halitasita kuwafutia mitihani wote watakaojihusisha na udanganyifu, wasimamizi wa mitihani wajiepushe na vitendo vya udanganyifu, atakayekiuka atachukuliwa hatua za kisheria.” alisema Msonde.
Kidato cha Nne Waanza Kufanya Mtihani wa Taifa Leo
0
October 30, 2017
Tags