Kigogo TRA Apandishwa Kizimbani

Kigogo TRA Apandishwa Kizimbani
Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kumiliki mali ambazo ni magari 19 na kuishi maisha ya kifahari kinyume na mshahara wake

Mshtakiwa amesomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambaye alidai mshtakiwa ana makosa mawili.
Alidai kuwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam, akiwa mwajiriwa wa TRA, kama Afisa Msaidizi wa Forodha alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikutwa akimiliki magari 19 ambayo ni Toyota RAV4, Toyota Dyna Truck, Toyota Vitz, Suzuki Carry,Toyota Ipsum, Toyota Wish,Toyota Mark ll, Toyota Regiusage, Toyota Estima, Toyota Alex, Toyota Noah, Toyota Crown, Toyota Hiace, Toyota Estima, Toyota Lasso, Suzuki Carry, ambayo yana thamani ya Tsh. Milioni 197.6.
Kosa la pili, anadaiwa kuwa kati ya March 21, 2012 na March 30, 2016 jijini Dar es Salaam akiwa mwajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu yenye thamani ya Tsh. 333,255,556.24 tofauti na kipato chake.
Wakili Peter amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo anaomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea maelezo ya awali (PH).
Hata hivyo, upande wa utetezi kupitia Wakili Elisalia Mosha aliiomba Mahakama hiyo kumpa dhamana mteja wake kwa sababu mashtaka aliyonayo yanadhaminiika kisheria.
Hakimu Shaidi alimtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Tsh. Milioni 20 ambapo alikidhi masharti na kuachiwa huru kwa dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Novemba 7, 2017.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa mfano watu wanaoishi kidiza kwa kuiibia serikali wawe kama 50 hivi unafikiria vipi wewe mtu mmoja magari 19 peke yako achilia majumba mshahara unaopata ni mbuzi kweli binadamu ni kiumbe mkatili sana bila ya aibu wala soni anamkodisha wakili wa kumtetea mahakamani kama vile eti anaonewa bure hahahahahaaaa balaa duniani

    ReplyDelete
  2. Vyote vinawezekana atakama unamshahara kidogo ni kujipanga tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. HAPO NI RUSHWA NA WIZI MTUPU, HAKUNA CHA KUJIPANGA WALA NENE

      Delete
  3. Maisha haya ya kiwizi-wizi ndio wapigaji wanayataka, wakibanwa kidogo utasikia 'maisha-magumu' mfyuuuuuuu. Dawa yao ni kufilisiwa na kutupwa jela maisha, na kazi ngumu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad