Kigwangala Asema Serikali Haiko Tayari Kuwavumilia Watendaji Wazembe

Kigwangala Asema Serikali Haiko Tayari Kuwavumilia Watendaji Wazembe
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangala, amesema serikali haitaweza kuwavumilia watendaji wazembe kwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Waziri Kigwangala ameandika hayo kwenye ukurasa wake wa instagrama, ambapo ameeleza kwamba watendaji hao wanachelewesha maendeleo ya nchi, hivyo watafikisha taarifa kwa mwenye mamlaka zaidi ili wachukuliwe hatua.
“Halmashauri chache zenye viongozi na watendaji wazembe zitabaki nyuma. zitatuangusha. Hatuko tayari kuvumilia, tutapendekeza kwa mwenye mamlaka hatua kali zichukuliwe”, ameandika Dkt. Kigwangala.
Dkt. Kigwangala ameendelea kwa kuandika kwamba kutokana na watu hao wanaingiwa na mashaka kuwaacha wasimamie miradi mikubwa ambayo inapaswa kutekelezwa, ikiwemo uboreshaji wa vituo vya afya, kitendo ambacho kinawatesa wananchi.
“Wizara ya Afya tumepata wafadhili ambao watatuwezesha kuboresha vituo vya Afya150 kwa kupeleka milioni za kitanzania 500 kwenye kila Kituo. Pesa hizi bado hazijaenda kwenye halmashauri mpaka sasa. Nachelea kusema tukiwapelekea viongozi na watendaji wa namna hii wanaweza kushindwa kuzisimamia ipasavyo, kuacha kupeleka ni kuwaadhibu wananchi wasio na hatia”, ameandika Dkt. Hamisi Kigwangala.
Hivi karibuni waziri Kigwangala amekuwa akifanya ziara kwenye vito vya afya mbali mbali nchini, kutathmini changamoto ambazo zinavikabili na kuvitafutia njia za ufumbuzi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad