Kiongozi wa Chadema Akwamatwa na Polisi

Kiongozi  wa Chadema Akwamatwa na Polisi
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduma, Herode Jivava ametiwa nguvuni na Polisi akidaiwa kutishia kuua kwa maneno.

Jivava ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Songwe anakuwa kiongozi wa nane kukamatwa na kuwekwa mahabusu. Baadhi ya waliokamatwa  wamefunguliwa kesi mahakamani na wengine wako nje kwa dhamana wakisubiri upelelezi wa polisi kukamilika.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu kukamatwa kwa Jivava, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo amesema alikamatwa jana Jumapili jioni mjini Vwawa akijiandaa kuingia uwanjani kuangalia mpira na alipelekwa Kituo cha Polisi Tunduma.

“Asubuhi hii tumefika hapa Polisi tumeambiwa Jivava anatuhumiwa kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno. Eti aliwatishia mgambo wakati wakiwaondoa kwa nguvu Machinga mjini Tunduma,” amesema.

 Sikagonamo amesema wanamsubiri mwanasheria ili kushughulikia suala hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange hakuwa tayari kuzungumzia taarifa za kukamatwa kwa Jivava akimtaka mwandishi wa Mwananchi kusubiri ili afuatilie tukio hilo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. waliotishia hadharani kwa kumtolea Nape ingawa walionekana Hawakushikwa.
    Waliotoa kauli na picha na simu kumuua lisu hawajashikwa.
    Ni mwanachadema tu mpinzani ndiye anayeonekana.
    Hata watoto wadogo wanaanza kuuliza, Je Ni Wanachadema tu ndo Wanaoonekana. Ndio maana wengi wanakwenda CCM. Huko hakuna mwenye makosa.Wote ni watakatifu .

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad