Kisa Kinguo Kifupi...Mrembo Prety Kindy Azomewa Mtaani

MSANII wa filamu Bongo, Suzan Michael maarufu kama Pretykind, juzikati alionja joto la jiwe baada ya kuzomewa na wanafunzi pamoja na watu wengine kufuatia kimini alichokivaa na kukatiza katika mitaa ya Tandale jijini Dar.
Muigizaji huyo alionekana akikatiza barabarani bila woga licha ya kuwa watu walikuwa wakimshangaa na kumcheka na kibaya zaidi wanafunzi wa shule waliokuwa wakikatiza eneo hilo walikuwa wakimzomea.
Lakini katika hali ya kushangaza, Pretykind alipotafutwa na kuulizwa juu ya tukio hilo alisema; “Sioni cha ajabu hapo, maana hayo ndiyo mavazi niliyozoea, nafanya kitu roho inapenda, uzuri nilikuwa na gari nikapaki mara moja kwenda dukani, nilivyoona watu wanaanza kujaa nikakimbilia kwenye gari.”

Stori: Mayasa Mariwata.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad